وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ ءَايَاتُنَا بَيِّنَٰتٍ قَالَ ٱلَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَآءَنَا ٱئْتِ بِقُرْءَانٍ غَيْرِ هَٰذَآ أَوْ بَدِّلْهُ قُلْ مَا يَكُونُ لِىٓ أَنْ أُبَدِّلَهُۥ مِن تِلْقَآئِ نَفْسِىٓ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَىَّ إِنِّىٓ أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّى عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasiotaraji kukutana na Sisi husema, “Leta Qur-ani isiyokuwa hii, au ibadilishe.” Sema, “Haiwi kwangu niibadilishe nitakavyo mimi mwenyewe. Mimi sifuati isipokuwa yale ninayofunuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi ninahofu, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasio taraji kukutana na Sisi husema: Lete Qur'ani isiyo kuwa hii, au ibadilishe. Sema: Hainifalii mimi kuibadilisha kwa nitakavyo nafsi yangu. Mimi sifuati ila ninayo funuliwa kwa Wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo kuu.