caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Yunus, Aya 71

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 51 · 10:71

وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِۦ يَٰقَوْمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِى وَتَذْكِيرِى بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوٓا۟ أَمْرَكُمْ وَشُرَكَآءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ ٱقْضُوٓا۟ إِلَىَّ وَلَا تُنظِرُونِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wasomee habari za Nuhu alipowaambia kaumu yake: Enyi kaumu yangu! Ikiwa ni kukubwa kwenu kukaa kwangu nanyi na kuwakumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu, basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, nyinyi likusanyeni jambo lenu pamoja na washirika wenu, kisha jambo lenu hilo lisiwe la kufichikana kwenu, kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70