caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura At-Tawba التوبة

Aya 129 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 113

بَرَآءَةٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation Center[Huku ni] kujiweka mbali kutokako kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwaendea wale mlioagana nao miongoni mwa washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسِيحُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِى ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱللَّهَ مُخْزِى ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tembeeni katika ardhi miezi minne, na jueni kwamba nyinyi hamwezi kumshinda Mwenyezi Mungu, na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawahizi makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَذَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوْمَ ٱلْحَجِّ ٱلْأَكْبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِىٓءٌ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ وَرَسُولُهُۥ فَإِن تُبْتُمْ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّكُمْ غَيْرُ مُعْجِزِى ٱللَّهِ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni tangazo kutoka kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kuwaendea watu wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu yuko mbali na washirikina, na Mtume wake pia yuko mbali. Kwa hivyo, mkitubu, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkigeuka, basi jueni kuwa nyinyi hamuwezi kumshinda Mwenyezi Mungu. Na wabashirie wale waliokufuru adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ثُمَّ لَمْ يَنقُصُوكُمْ شَيْـًٔا وَلَمْ يُظَٰهِرُوا۟ عَلَيْكُمْ أَحَدًا فَأَتِمُّوٓا۟ إِلَيْهِمْ عَهْدَهُمْ إِلَىٰ مُدَّتِهِمْ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIsipokuwa wale mlioagana nao katika washirikina, kisha hawakuwapunguza chochote, wala hawakumsaidia yeyote dhidi yenu. Basi hao watimizieni ahadi yao mpaka muda wao. Hakika, Mwenyezi Mungu huwapenda wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِذَا ٱنسَلَخَ ٱلْأَشْهُرُ ٱلْحُرُمُ فَٱقْتُلُوا۟ ٱلْمُشْرِكِينَ حَيْثُ وَجَدتُّمُوهُمْ وَخُذُوهُمْ وَٱحْصُرُوهُمْ وَٱقْعُدُوا۟ لَهُمْ كُلَّ مَرْصَدٍ فَإِن تَابُوا۟ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَخَلُّوا۟ سَبِيلَهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiisha miezi mitukufu, basi waueni washirikina popote muwakutapo, na wachukueni na wazingireni, na wavizieni katika kila njia. Lakini wakitubu, na wakashika Sala, na wakatoa Zaka, basi waachilieni njia yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِنْ أَحَدٌ مِّنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ٱسْتَجَارَكَ فَأَجِرْهُ حَتَّىٰ يَسْمَعَ كَلَٰمَ ٱللَّهِ ثُمَّ أَبْلِغْهُ مَأْمَنَهُۥ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa yeyote miongoni mwa washirikina atakuomba ulinzi, basi mpe ulinzi ili apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe mahali pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni kaumu wasiojua kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ رَسُولِهِۦٓ إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّمْ عِندَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ فَمَا ٱسْتَقَٰمُوا۟ لَكُمْ فَٱسْتَقِيمُوا۟ لَهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVipi washirikina watakuwa na agano kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake, isipokuwa wale mliofanya agano nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu watawawia wanyoofu, basi nanyi pia wawieni wanyoofu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا۟ عَلَيْكُمْ لَا يَرْقُبُوا۟ فِيكُمْ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً يُرْضُونَكُم بِأَفْوَٰهِهِمْ وَتَأْبَىٰ قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَٰسِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterVipi, na wakiwa na ushindi dhidi yenu, hawachungi kwenu udugu wala ahadi. Wanawafurahisha kwa midomo yao tu, lakini nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱشْتَرَوْا۟ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَصَدُّوا۟ عَن سَبِيلِهِۦٓ إِنَّهُمْ سَآءَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalinunua Ishara za Mwenyezi Mungu kwa thamani chache, kwa hivyo wakaizuilia njia yake. Hakika hao ni maovu waliyokuwa wakiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يَرْقُبُونَ فِى مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُعْتَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawachungi kwa Muumini udugu wala ahadi. Basi hao ndio wapindukiao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِن تَابُوا۟ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَوُا۟ ٱلزَّكَوٰةَ فَإِخْوَٰنُكُمْ فِى ٱلدِّينِ وَنُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo wakitubu, na wakasimamisha Sala, na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini. Na tunazipambanua Aya kwa kaumu wanaojua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن نَّكَثُوٓا۟ أَيْمَٰنَهُم مِّنۢ بَعْدِ عَهْدِهِمْ وَطَعَنُوا۟ فِى دِينِكُمْ فَقَٰتِلُوٓا۟ أَئِمَّةَ ٱلْكُفْرِ إِنَّهُمْ لَآ أَيْمَٰنَ لَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَنتَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakivunja viapo vyao baada ya agano lao, na wakaitia dosari Dini yenu, basi piganeni na viongozi wa ukafiri. Hakika hao hawana viapo vya kweli. Huenda (kwa hayo) wakaacha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَا تُقَٰتِلُونَ قَوْمًا نَّكَثُوٓا۟ أَيْمَٰنَهُمْ وَهَمُّوا۟ بِإِخْرَاجِ ٱلرَّسُولِ وَهُم بَدَءُوكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ أَتَخْشَوْنَهُمْ فَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَوْهُ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hampigani na kaumu waliovunja viapo vyao na wakawa na hamu ya kumtoa Mtume, nao ndio waliowaanza mara ya kwanza? Je, mnawaogopa? Basi Mwenyezi Mungu anastahiki zaidi mumwogope, ikiwa nyinyi ni Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَٰتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ ٱللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterPiganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na awanusuru dhidi yao, na aviponye vifua vya kaumu ya Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيُذْهِبْ غَيْظَ قُلُوبِهِمْ وَيَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa aondoe hasira ya nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu humkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تُتْرَكُوا۟ وَلَمَّا يَعْلَمِ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ جَٰهَدُوا۟ مِنكُمْ وَلَمْ يَتَّخِذُوا۟ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلَا رَسُولِهِۦ وَلَا ٱلْمُؤْمِنِينَ وَلِيجَةً وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mlidhani kuwa mtaachwa tu, na Mwenyezi Mungu hajawajua wale waliopigana Jihadi miongoni mwenu, na wala hawakumfanya yeyote mwendani wao isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Waumini wenziwe? Na Mwenyezi Mungu anazo habari za yote mnayoyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا كَانَ لِلْمُشْرِكِينَ أَن يَعْمُرُوا۟ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ شَٰهِدِينَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِم بِٱلْكُفْرِ أُو۟لَٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَٰلُهُمْ وَفِى ٱلنَّارِ هُمْ خَٰلِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaikuwa kwa washirikina kwamba waiimarishe misikiti ya Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa wanazishuhudia nafsi zao wenyewe ukafiri. Hao matendo yao yaliharibika, na katika Moto wao watadumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا يَعْمُرُ مَسَٰجِدَ ٱللَّهِ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَأَقَامَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتَى ٱلزَّكَوٰةَ وَلَمْ يَخْشَ إِلَّا ٱللَّهَ فَعَسَىٰٓ أُو۟لَٰٓئِكَ أَن يَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُهْتَدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika anayeimarisha tu misikiti ya Mwenyezi Mungu ni yule anayemwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akasimamisha Sala, na akatoa Zaka, na wala hakumnyenyekea isipokuwa Mwenyezi Mungu. Basi huenda hao wakawa katika waongofu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ ٱلْحَآجِّ وَعِمَارَةَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ كَمَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَجَٰهَدَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا يَسْتَوُۥنَ عِندَ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mnafanya kuwanywesha maji Mahujaji na kuimarisha Msikiti Mtakatifu ni sawa na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَهَاجَرُوا۟ وَجَٰهَدُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ ٱللَّهِ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَآئِزُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale walioamini, na wakahama, na wakafanya Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, hao wana daraja kubwa zaidi kwa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofuzu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَٰنٍ وَجَنَّٰتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wao Mlezi anawabashiria rehema zitokazo kwake, na radhi, na Bustani ambazo humo wana neema za kudumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجْرٌ عَظِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatadumu humo milele. Hakika kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo makubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوٓا۟ ءَابَآءَكُمْ وَإِخْوَٰنَكُمْ أَوْلِيَآءَ إِنِ ٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْكُفْرَ عَلَى ٱلْإِيمَٰنِ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa marafiki walinzi wenu ikiwa wanaupendelea ukafiri kuliko Imani. Na mwenye kuwafanya marafiki walinzi miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِن كَانَ ءَابَآؤُكُمْ وَأَبْنَآؤُكُمْ وَإِخْوَٰنُكُمْ وَأَزْوَٰجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَٰلٌ ٱقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَٰرَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَٰكِنُ تَرْضَوْنَهَآ أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَجِهَادٍ فِى سَبِيلِهِۦ فَتَرَبَّصُوا۟ حَتَّىٰ يَأْتِىَ ٱللَّهُ بِأَمْرِهِۦ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَٰسِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ikiwa baba zenu, na wana wenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mlizozichuma, na biashara mnazohofia kuharibika kwake, na makazi mnayoyaridhia, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu aje na amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدْ نَصَرَكُمُ ٱللَّهُ فِى مَوَاطِنَ كَثِيرَةٍ وَيَوْمَ حُنَيْنٍ إِذْ أَعْجَبَتْكُمْ كَثْرَتُكُمْ فَلَمْ تُغْنِ عَنكُمْ شَيْـًٔا وَضَاقَتْ عَلَيْكُمُ ٱلْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ ثُمَّ وَلَّيْتُم مُّدْبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu aliwanusuru katika maeneo mengi, na siku ya Hunayni wakati wingi wenu uliwapa majivuno, lakini haukuwafaa kitu, na ardhi ikawa finyu kwenu pamoja na upana wake. Kisha mkageuka mkapeana migongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ أَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَعَلَى ٱلْمُؤْمِنِينَ وَأَنزَلَ جُنُودًا لَّمْ تَرَوْهَا وَعَذَّبَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha Mwenyezi Mungu akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya Waumini. Na akateremsha majeshi ambayo hamkuyaona, na akawaadhibu wale waliokufuru. Na hayo ndiyo malipo ya makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ يَتُوبُ ٱللَّهُ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu atamkubalia toba amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe dhambi, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّمَا ٱلْمُشْرِكُونَ نَجَسٌ فَلَا يَقْرَبُوا۟ ٱلْمَسْجِدَ ٱلْحَرَامَ بَعْدَ عَامِهِمْ هَٰذَا وَإِنْ خِفْتُمْ عَيْلَةً فَسَوْفَ يُغْنِيكُمُ ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦٓ إِن شَآءَ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Hakika washirikina ni najisi, kwa hivyo wasiukaribie Msikiti Mtakatifu baada ya mwaka wao huu. Na ikiwa mnahofia umasikini, basi Mwenyezi Mungu atakutajirisheni kutoka katika fadhila zake akitaka. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَٰتِلُوا۟ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَلَا يُحَرِّمُونَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَلَا يَدِينُونَ دِينَ ٱلْحَقِّ مِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ حَتَّىٰ يُعْطُوا۟ ٱلْجِزْيَةَ عَن يَدٍ وَهُمْ صَٰغِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterPiganeni na wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho, wala hawaharamishi yale aliyoharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawashiki Dini ya haki, miongoni mwa wale waliopewa Kitabu, mpaka watoe kodi kwa hiari yao, hali wametii.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَتِ ٱلْيَهُودُ عُزَيْرٌ ٱبْنُ ٱللَّهِ وَقَالَتِ ٱلنَّصَٰرَى ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ ٱللَّهِ ذَٰلِكَ قَوْلُهُم بِأَفْوَٰهِهِمْ يُضَٰهِـُٔونَ قَوْلَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن قَبْلُ قَٰتَلَهُمُ ٱللَّهُ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mayahudi walisema: Uzeir ni mwana wa Mwenyezi Mungu. Na Wakristo walisema: Masihi ni mwana wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ni kauli yao tu kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya wale waliokufuru kabla yao. Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱتَّخَذُوٓا۟ أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَٰنَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَٱلْمَسِيحَ ٱبْنَ مَرْيَمَ وَمَآ أُمِرُوٓا۟ إِلَّا لِيَعْبُدُوٓا۟ إِلَٰهًا وَٰحِدًا لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ سُبْحَٰنَهُۥ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaliwafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni mabwana badala ya Mwenyezi Mungu, na pia Masihi mwana wa Maryamu. Na wala hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Mungu Mmoja, hakuna mungu isipokuwa Yeye. Subhanahu (ametakasika) mbali na hayo wanayoyashirikisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُرِيدُونَ أَن يُطْفِـُٔوا۟ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفْوَٰهِهِمْ وَيَأْبَى ٱللَّهُ إِلَّآ أَن يُتِمَّ نُورَهُۥ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa isipokuwa aitimize Nuru yake hata makafiri wakichukia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِىٓ أَرْسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلْهُدَىٰ وَدِينِ ٱلْحَقِّ لِيُظْهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْمُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili aipe ushindi juu ya dini zote, hata washirikina wakichukia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلْأَحْبَارِ وَٱلرُّهْبَانِ لَيَأْكُلُونَ أَمْوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلْبَٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلَّذِينَ يَكْنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa batili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Na wale wanaolimbika dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika Njia ya Mwenyezi Mungu, basi wabashirie adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ يُحْمَىٰ عَلَيْهَا فِى نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكْوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمْ وَجُنُوبُهُمْ وَظُهُورُهُمْ هَٰذَا مَا كَنَزْتُمْ لِأَنفُسِكُمْ فَذُوقُوا۟ مَا كُنتُمْ تَكْنِزُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku zitakapotiwa moto katika Moto wa Jahannamu, na kwazo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, wakaambiwa: Haya ndiyo mliyozilimbikia nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkilimbika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِى كِتَٰبِ ٱللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ مِنْهَآ أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ فَلَا تَظْلِمُوا۟ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ وَقَٰتِلُوا۟ ٱلْمُشْرِكِينَ كَآفَّةً كَمَا يُقَٰتِلُونَكُمْ كَآفَّةً وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na miwili katika andiko la Mwenyezi Mungu tangu alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko minne mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wanavyopigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا ٱلنَّسِىٓءُ زِيَادَةٌ فِى ٱلْكُفْرِ يُضَلُّ بِهِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُحِلُّونَهُۥ عَامًا وَيُحَرِّمُونَهُۥ عَامًا لِّيُوَاطِـُٔوا۟ عِدَّةَ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ فَيُحِلُّوا۟ مَا حَرَّمَ ٱللَّهُ زُيِّنَ لَهُمْ سُوٓءُ أَعْمَٰلِهِمْ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika kuahirisha (miezi) ni kuzidi tu katika kukufuru; wanapotezwa kwa hilo wale waliokufuru. Wanauhalalisha mwaka mmoja na kuharimisha mwaka mwingine, ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyoitukuza Mwenyezi Mungu, ndiyo wahalalishe yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu. Wamepambiwa ubaya wa vitendo vyao hivi. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ٱنفِرُوا۟ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱثَّاقَلْتُمْ إِلَى ٱلْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا مِنَ ٱلْـَٔاخِرَةِ فَمَا مَتَٰعُ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mna nini mnapoambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kwa kulinganisha na Akhera siyo isipokuwa chache.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا تَنفِرُوا۟ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْـًٔا وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKama hamuendi, atawaadhibu adhabu chungu, na atawabadilisha na kaumu wasiokuwa nyinyi, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا تَنصُرُوهُ فَقَدْ نَصَرَهُ ٱللَّهُ إِذْ أَخْرَجَهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ثَانِىَ ٱثْنَيْنِ إِذْ هُمَا فِى ٱلْغَارِ إِذْ يَقُولُ لِصَٰحِبِهِۦ لَا تَحْزَنْ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَنَا فَأَنزَلَ ٱللَّهُ سَكِينَتَهُۥ عَلَيْهِ وَأَيَّدَهُۥ بِجُنُودٍ لَّمْ تَرَوْهَا وَجَعَلَ كَلِمَةَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ٱلسُّفْلَىٰ وَكَلِمَةُ ٱللَّهِ هِىَ ٱلْعُلْيَا وَٱللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIkiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwishamnusuru walipomtoa wale waliokufuru, akiwa ni wa pili wa wawili walipokuwa katika pango, alipomwambia sahibu yake: 'Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi.' Basi Mwenyezi Mungu akauteremsha utulivu wake juu yake, na akamuunga mkono kwa majeshi ambayo hamkuyaona, na akalifanya neno la wale waliokufuru kuwa chini zaidi, na Neno la Mwenyezi Mungu ndilo la juu zaidi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱنفِرُوا۟ خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTokeni muende mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali zenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hayo ni heri kwenu ikiwa mnajua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَوْ كَانَ عَرَضًا قَرِيبًا وَسَفَرًا قَاصِدًا لَّٱتَّبَعُوكَ وَلَٰكِنۢ بَعُدَتْ عَلَيْهِمُ ٱلشُّقَّةُ وَسَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَوِ ٱسْتَطَعْنَا لَخَرَجْنَا مَعَكُمْ يُهْلِكُونَ أَنفُسَهُمْ وَٱللَّهُ يَعْلَمُ إِنَّهُمْ لَكَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLau ingelikuwa ipo faida ya papo kwa hapo, na safari fupi, basi hakika wangelikufuata. Lakini waliona kwamba ni mbali na kuna ugumu. Nao wataapa kwa Mwenyezi Mungu: 'Tungeliweza, basi bila ya shaka tungelitoka pamoja nanyi.' Wanaziangamiza nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa hakika hao ni waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَفَا ٱللَّهُ عَنكَ لِمَ أَذِنتَ لَهُمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكَ ٱلَّذِينَ صَدَقُوا۟ وَتَعْلَمَ ٱلْكَٰذِبِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amekusamehe! Kwa nini ukawapa ruhusa kabla ya kukubainikia wale wanaosema ukweli, na ukawajua waongo?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يَسْتَـْٔذِنُكَ ٱلَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ أَن يُجَٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawakuombi ruhusa wale wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho ili wafanye Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا يَسْتَـْٔذِنُكَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَٱرْتَابَتْ قُلُوبُهُمْ فَهُمْ فِى رَيْبِهِمْ يَتَرَدَّدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wanakuomba ruhusa tu wale wasiomwamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na nyoyo zao zikatia shaka. Basi hao wanasitasita katika shaka yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ أَرَادُوا۟ ٱلْخُرُوجَ لَأَعَدُّوا۟ لَهُۥ عُدَّةً وَلَٰكِن كَرِهَ ٱللَّهُ ٱنۢبِعَاثَهُمْ فَثَبَّطَهُمْ وَقِيلَ ٱقْعُدُوا۟ مَعَ ٱلْقَٰعِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wangelitaka kweli kutoka, basi bila ya shaka wangeliliandalia hilo maandalizi ya sawasawa. Lakini Mwenyezi Mungu alichukia kutoka kwao, kwa hivyo akawazuia na ikasemwa: Kaeni pamoja na wanaokaa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَوْ خَرَجُوا۟ فِيكُم مَّا زَادُوكُمْ إِلَّا خَبَالًا وَلَأَوْضَعُوا۟ خِلَٰلَكُمْ يَبْغُونَكُمُ ٱلْفِتْنَةَ وَفِيكُمْ سَمَّٰعُونَ لَهُمْ وَٱللَّهُ عَلِيمٌۢ بِٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLau wangelitoka kati yenu, wasingeliwazidisha isipokuwa mchafuko, na wangetangatanga kati yenu wakiwatakia fitina. Na miongoni mwenu wako wanaowasikiliza sana. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدِ ٱبْتَغَوُا۟ ٱلْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُوا۟ لَكَ ٱلْأُمُورَ حَتَّىٰ جَآءَ ٱلْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ ٱللَّهِ وَهُمْ كَٰرِهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika, walikwishataka kuleta mafarakano tangu zamani, na wakakugeuzia mambo, mpaka ikaja haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu hali kuwa wao wamechukia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْهُم مَّن يَقُولُ ٱئْذَن لِّى وَلَا تَفْتِنِّىٓ أَلَا فِى ٱلْفِتْنَةِ سَقَطُوا۟ وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمُحِيطَةٌۢ بِٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao wapo wanaosema: 'Niruhusu wala usinitie majaribuni.' Kwa yakini wao hivyo wamekwishatumbukia katika majaribu. Na hakika Jahannam imewazingira makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِن تُصِبْكَ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكَ مُصِيبَةٌ يَقُولُوا۟ قَدْ أَخَذْنَآ أَمْرَنَا مِن قَبْلُ وَيَتَوَلَّوا۟ وَّهُمْ فَرِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLikikupata zuri, linawawia baya. Na ukikusibu msiba, wanasema: 'Sisi hakika tuliangalia mambo yetu vizuri tangu zamani.' Na wanageuka kwenda zao hali ya kuwa wamefurahi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُل لَّن يُصِيبَنَآ إِلَّا مَا كَتَبَ ٱللَّهُ لَنَا هُوَ مَوْلَىٰنَا وَعَلَى ٱللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Halitusibu isipokuwa yale aliyotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na kwa Mwenyezi Mungu, basi na wategemee Waumini!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ هَلْ تَرَبَّصُونَ بِنَآ إِلَّآ إِحْدَى ٱلْحُسْنَيَيْنِ وَنَحْنُ نَتَرَبَّصُ بِكُمْ أَن يُصِيبَكُمُ ٱللَّهُ بِعَذَابٍ مِّنْ عِندِهِۦٓ أَوْ بِأَيْدِينَا فَتَرَبَّصُوٓا۟ إِنَّا مَعَكُم مُّتَرَبِّصُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hivyo mnatutazamia litupate lolote isipokuwa moja katika mazuri mawili? Na sisi tunawatazamia kuwa Mwenyezi Mungu atawasibu kwa adhabu kutoka kwake, au kwa mikono yetu. Basi tazamieni, nasi hakika tunatazamia pamoja nanyi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ أَنفِقُوا۟ طَوْعًا أَوْ كَرْهًا لَّن يُتَقَبَّلَ مِنكُمْ إِنَّكُمْ كُنتُمْ قَوْمًا فَٰسِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Toeni kwa kupenda au kwa kuchukia. Kamwe hakitakubaliwa kutoka kwenu. Kwani hakika nyinyi mmekuwa kaumu wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَٰتُهُمْ إِلَّآ أَنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأْتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَٰرِهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hawakuzuiliwa kukubaliwa kutoa kwao isipokuwa kwa kuwa walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala hawaji kwenye Sala isipokuwa huku ni wavivu, wala hawatoi isipokuwa nao wamechukia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَٰلُهُمْ وَلَآ أَوْلَٰدُهُمْ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi zisikufurahishe mali zao wala wana wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwazo katika maisha ya dunia hii, na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنَّهُمْ لَمِنكُمْ وَمَا هُم مِّنكُمْ وَلَٰكِنَّهُمْ قَوْمٌ يَفْرَقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanaapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba wao ni katika nyinyi, wala wao si katika nyinyi. Lakini wao ni kaumu wanaoogopa mno.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَوْ يَجِدُونَ مَلْجَـًٔا أَوْ مَغَٰرَٰتٍ أَوْ مُدَّخَلًا لَّوَلَّوْا۟ إِلَيْهِ وَهُمْ يَجْمَحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLau kama watapata pa kukimbilia au mapango au mahali pa kuingia, basi hakika wangeligeuka kwenda huko huku wanakimbia mbio zisizozuilika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْهُم مَّن يَلْمِزُكَ فِى ٱلصَّدَقَٰتِ فَإِنْ أُعْطُوا۟ مِنْهَا رَضُوا۟ وَإِن لَّمْ يُعْطَوْا۟ مِنْهَآ إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao kuna yule anayekusengenya kuhusiana na sadaka. Kwa hivyo wakipewa kwayo, wanaridhika. Na wasipopewa kwayo, tazama, wanakasirika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ أَنَّهُمْ رَضُوا۟ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَقَالُوا۟ حَسْبُنَا ٱللَّهُ سَيُؤْتِينَا ٱللَّهُ مِن فَضْلِهِۦ وَرَسُولُهُۥٓ إِنَّآ إِلَى ٱللَّهِ رَٰغِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau kuwa waliridhia kile alichowapa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakasema: Mwenyezi Mungu anatutosheleza, Mwenyezi Mungu atatupa katika fadhila yake, na pia Mtume wake; hakika sisi ni wenye kumtaka Mwenyezi Mungu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا ٱلصَّدَقَٰتُ لِلْفُقَرَآءِ وَٱلْمَسَٰكِينِ وَٱلْعَٰمِلِينَ عَلَيْهَا وَٱلْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِى ٱلرِّقَابِ وَٱلْغَٰرِمِينَ وَفِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ فَرِيضَةً مِّنَ ٱللَّهِ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika sadaka ni za mafakiri tu, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na waliogharamika, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu uliofaridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْهُمُ ٱلَّذِينَ يُؤْذُونَ ٱلنَّبِىَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَٱلَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ ٱللَّهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao kuna wale wanaomuudhi Nabii na wanasema: Yeye ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la heri kwenu. Anamwamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanaoamini miongoni mwenu. Na wale wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu wana adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمْ لِيُرْضُوكُمْ وَٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَحَقُّ أَن يُرْضُوهُ إِن كَانُوا۟ مُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanawaapia kwa Mwenyezi Mungu ili wakuridhishenyi, ilhali Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanaostahiki zaidi kwamba wao wawaridhishe ikiwa wao ni Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّهُۥ مَن يُحَادِدِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَأَنَّ لَهُۥ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدًا فِيهَا ذَٰلِكَ ٱلْخِزْىُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawajui ya kwamba anayempinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo hakika ana Moto wa Jahannam adumu humo? Hiyo ndiyo hizaya kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَحْذَرُ ٱلْمُنَٰفِقُونَ أَن تُنَزَّلَ عَلَيْهِمْ سُورَةٌ تُنَبِّئُهُم بِمَا فِى قُلُوبِهِمْ قُلِ ٱسْتَهْزِءُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ مُخْرِجٌ مَّا تَحْذَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanafiki wanaogopa kwamba iteremshwe Sura juu yao itakayowaambia yale yaliyo katika nyoyo zao. Sema: Fanyeni stihizai! Hakika Mwenyezi Mungu atayatoa nje hayo mnayoyaogopa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ قُلْ أَبِٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ وَرَسُولِهِۦ كُنتُمْ تَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Kwani mlikuwa mkimfanyia masikhara Mwenyezi Mungu, na ishara zake, na Mtume wake?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا تَعْتَذِرُوا۟ قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَٰنِكُمْ إِن نَّعْفُ عَن طَآئِفَةٍ مِّنكُمْ نُعَذِّبْ طَآئِفَةًۢ بِأَنَّهُمْ كَانُوا۟ مُجْرِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMsitoe udhuru. Hakika mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja miongoni mwenu, tunaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao wamekuwa wahalifu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْمُنَٰفِقُونَ وَٱلْمُنَٰفِقَٰتُ بَعْضُهُم مِّنۢ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِٱلْمُنكَرِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمَعْرُوفِ وَيَقْبِضُونَ أَيْدِيَهُمْ نَسُوا۟ ٱللَّهَ فَنَسِيَهُمْ إِنَّ ٱلْمُنَٰفِقِينَ هُمُ ٱلْفَٰسِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanaume wanafiki na wanawake wanafiki, wote ni hali moja. Huamrisha maovu na hukataza mema, na huifumba mikono yao. Walimsahau Mwenyezi Mungu, basi na Yeye pia akawasahau. Hakika wanafiki ndio wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْمُنَٰفِقِينَ وَٱلْمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلْكُفَّارَ نَارَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَا هِىَ حَسْبُهُمْ وَلَعَنَهُمُ ٱللَّهُ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّقِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannamu watadumu humo. Hiyo ndiyo inawatosha, na Mwenyezi Mungu amewalaani; nao wana adhabu ya kudumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ كَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنكُمْ قُوَّةً وَأَكْثَرَ أَمْوَٰلًا وَأَوْلَٰدًا فَٱسْتَمْتَعُوا۟ بِخَلَٰقِهِمْ فَٱسْتَمْتَعْتُم بِخَلَٰقِكُمْ كَمَا ٱسْتَمْتَعَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِكُم بِخَلَٰقِهِمْ وَخُضْتُمْ كَٱلَّذِى خَاضُوٓا۟ أُو۟لَٰٓئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَٰلُهُمْ فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَٰسِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi kama wale waliokuwa kabla yenu. Walikuwa wana nguvu na mali na watoto zaidi kuwaliko nyinyi. Basi walistareheka kwa fungu lao, na nyinyi mnastareheka kwa fungu lenu, kama walivyostareheka kwa fungu lao wale waliokuwa kabla yenu. Na nyinyi mkazama katika maovu kama wao walivyozama. Hao, matendo yao yaliharibika katika dunia na Akhera; na hao ndio waliohasiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ يَأْتِهِمْ نَبَأُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَقَوْمِ إِبْرَٰهِيمَ وَأَصْحَٰبِ مَدْيَنَ وَٱلْمُؤْتَفِكَٰتِ أَتَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hazikuwajia habari za wale waliokuwa kabla yao, kaumu ya Nuhu, na A'ad, na Thamud, na kaumu ya Ibrahim, na watu wa Madyana, na miji iliyopinduliwa chini juu? Mitume wao waliwajia na hoja zilizo wazi. Basi Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini wao walikuwa wakijidhulumu wenyewe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْمُؤْمِنُونَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤْتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَيُطِيعُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ أُو۟لَٰٓئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ ٱللَّهُ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na husimamisha Sala, na hutoa Zaka, na humtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ جَنَّٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةً فِى جَنَّٰتِ عَدْنٍ وَرِضْوَٰنٌ مِّنَ ٱللَّهِ أَكْبَرُ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Bustani zipitiazo mito chini yake, watadumu humo. Na makazi mema katika Bustani za kudumu, na Radhi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ndizo kubwa zaidi kuliko yote. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ جَٰهِدِ ٱلْكُفَّارَ وَٱلْمُنَٰفِقِينَ وَٱغْلُظْ عَلَيْهِمْ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ ٱلْمَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Nabii! Pambana na makafiri na wanafiki, na wawiye mgumu. Na makazi yao ni Jahannamu, na hayo ndiyo marejeo mabaya kabisa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ مَا قَالُوا۟ وَلَقَدْ قَالُوا۟ كَلِمَةَ ٱلْكُفْرِ وَكَفَرُوا۟ بَعْدَ إِسْلَٰمِهِمْ وَهَمُّوا۟ بِمَا لَمْ يَنَالُوا۟ وَمَا نَقَمُوٓا۟ إِلَّآ أَنْ أَغْنَىٰهُمُ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ مِن فَضْلِهِۦ فَإِن يَتُوبُوا۟ يَكُ خَيْرًا لَّهُمْ وَإِن يَتَوَلَّوْا۟ يُعَذِّبْهُمُ ٱللَّهُ عَذَابًا أَلِيمًا فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَمَا لَهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa hawakusema; nao hakika wamekwishasema neno la ukafiri, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakawa na utashi mkubwa juu ya yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia ila kwa kuwa Mwenyezi Mungu aliwatajirisha, na Mtume wake pia kutokana na fadhila zake. Basi wakitubu, itakuwa heri kwao. Na wakigeuka, Mwenyezi Mungu atawaadhibu adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na wala hawana katika ardhi mlinzi yeyote wala wa kuwanusuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْهُم مَّنْ عَٰهَدَ ٱللَّهَ لَئِنْ ءَاتَىٰنَا مِن فَضْلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّٰلِحِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa miongoni mwao kuwa wale waliomuahidi Mwenyezi Mungu kwamba: Akitupa katika fadhila yake, hapana shaka tutatoa sadaka, na tutakuwa katika waliotengenea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُم مِّن فَضْلِهِۦ بَخِلُوا۟ بِهِۦ وَتَوَلَّوا۟ وَّهُم مُّعْرِضُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipowapa katika fadhila yake, wakaifanyia ubahili na wakageuka hali ya kuwa wamepeana mgongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِى قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُۥ بِمَآ أَخْلَفُوا۟ ٱللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا۟ يَكْذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akawafuatisha unafiki katika nyoyo zao mpaka Siku watakapokutana naye, kwa sababu ya kuwa walimvunjia Mwenyezi Mungu yale waliyomuahidi, na kwa sababu ya kusema kwao uongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَعْلَمُ سِرَّهُمْ وَنَجْوَىٰهُمْ وَأَنَّ ٱللَّهَ عَلَّٰمُ ٱلْغُيُوبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawajui kwamba Mwenyezi Mungu anajua siri zao na minong'ono yao, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua sana ya ghaibu?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يَلْمِزُونَ ٱلْمُطَّوِّعِينَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ فِى ٱلصَّدَقَٰتِ وَٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ إِلَّا جُهْدَهُمْ فَيَسْخَرُونَ مِنْهُمْ سَخِرَ ٱللَّهُ مِنْهُمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wanaowabeua Waumini wanaotoa sadaka nyingi na wasio na cha kutoa ila kiasi cha juhudi yao, hivyo wanawafanyia masikhara. Mwenyezi Mungu atawakejeli wao! Nao wana adhabu chungu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱسْتَغْفِرْ لَهُمْ أَوْ لَا تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ إِن تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ سَبْعِينَ مَرَّةً فَلَن يَغْفِرَ ٱللَّهُ لَهُمْ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْفَٰسِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaombee msamaha au usiwaombee msamaha. Hata ukiwaombea msamaha mara sabini, Mwenyezi Mungu hatawasamehe. Hayo ni kwa sababu ya kuwa wao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَرِحَ ٱلْمُخَلَّفُونَ بِمَقْعَدِهِمْ خِلَٰفَ رَسُولِ ٱللَّهِ وَكَرِهُوٓا۟ أَن يُجَٰهِدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَقَالُوا۟ لَا تَنفِرُوا۟ فِى ٱلْحَرِّ قُلْ نَارُ جَهَنَّمَ أَشَدُّ حَرًّا لَّوْ كَانُوا۟ يَفْقَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalifurahi walioachwa nyuma kwa kule kukaa kwao nyuma ya Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na wakachukia kupigana Jihadi kwa mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wakasema: Msitoke kwenda katika joto! Sema: Moto wa Jahannamu una joto kubwa zaidi, laiti wangelikuwa wanafahamu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلْيَضْحَكُوا۟ قَلِيلًا وَلْيَبْكُوا۟ كَثِيرًا جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi na wacheke kidogo, na walie sana. Hayo ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِن رَّجَعَكَ ٱللَّهُ إِلَىٰ طَآئِفَةٍ مِّنْهُمْ فَٱسْتَـْٔذَنُوكَ لِلْخُرُوجِ فَقُل لَّن تَخْرُجُوا۟ مَعِىَ أَبَدًا وَلَن تُقَٰتِلُوا۟ مَعِىَ عَدُوًّا إِنَّكُمْ رَضِيتُم بِٱلْقُعُودِ أَوَّلَ مَرَّةٍ فَٱقْعُدُوا۟ مَعَ ٱلْخَٰلِفِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Mwenyezi Mungu akikurudisha kwenye kikundi kimoja miongoni mwao - na wakakutaka idhini ya kutoka - basi sema: Nyinyi hamtatoka pamoja nami kabisa, wala hamtapigana na adui pamoja nami. Hakika nyinyi mliridhia kusalia nyuma mara ya kwanza, basi kaeni pamoja na hao waliosalia nyuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰٓ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِۦٓ إِنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ فَٰسِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala usimsalie kabisa yeyote katika wao akifa, wala usisimame kaburini kwake. Hakika hao walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakafa hali ya kuwa wamevuka mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَٰلُهُمْ وَأَوْلَٰدُهُمْ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُعَذِّبَهُم بِهَا فِى ٱلدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala zisikupendeze mali zao na watoto wao. Hakika Mwenyezi Mungu anataka tu kuwaadhibu kwa hayo katika dunia; na zitoke roho zao hali ya kuwa ni makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ أَنْ ءَامِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَجَٰهِدُوا۟ مَعَ رَسُولِهِ ٱسْتَـْٔذَنَكَ أُو۟لُوا۟ ٱلطَّوْلِ مِنْهُمْ وَقَالُوا۟ ذَرْنَا نَكُن مَّعَ ٱلْقَٰعِدِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa inapoteremshwa sura kwamba muaminini Mwenyezi Mungu na piganeni Jihadi pamoja na Mtume wake, wale wenye nguvu miongoni mwao hukutaka ruhusa na wanasema: Tuache tuwe pamoja na wanaokaa nyuma!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَضُوا۟ بِأَن يَكُونُوا۟ مَعَ ٱلْخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَفْقَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWaliridhia kwamba wawe pamoja na wasaliao nyuma, na nyoyo zao zikafunikwa, kwa hivyo hawafahamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَٰكِنِ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ جَٰهَدُوا۟ بِأَمْوَٰلِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ وَأُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلْخَيْرَٰتُ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini Mtume na wale walioamini pamoja naye, walifanya Jihadi kwa mali zao na nafsi zao. Na hao ndio wana heri nyingi. Na hao ndio waliofaulu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُمْ جَنَّٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu amewaandalia Bustani zipitazo mito kwa chini yake, watadumu humo. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَجَآءَ ٱلْمُعَذِّرُونَ مِنَ ٱلْأَعْرَابِ لِيُؤْذَنَ لَهُمْ وَقَعَدَ ٱلَّذِينَ كَذَبُوا۟ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ سَيُصِيبُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walikuja wenye kutoa udhuru miongoni mwa Mabedui ili wapewe ruhusa, na wakakaa wale waliomdanganya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Itawafika wale waliokufuru miongoni mwao adhabu chungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّيْسَ عَلَى ٱلضُّعَفَآءِ وَلَا عَلَى ٱلْمَرْضَىٰ وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ لَا يَجِدُونَ مَا يُنفِقُونَ حَرَجٌ إِذَا نَصَحُوا۟ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦ مَا عَلَى ٱلْمُحْسِنِينَ مِن سَبِيلٍ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakuna lawama juu ya wanyonge, wala juu ya wagonjwa, wala juu ya wale wasiopata cha kutoa, maadamu wanamsafia nia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakuna njia ya kuwalaumu wanaofanya mazuri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا عَلَى ٱلَّذِينَ إِذَا مَآ أَتَوْكَ لِتَحْمِلَهُمْ قُلْتَ لَآ أَجِدُ مَآ أَحْمِلُكُمْ عَلَيْهِ تَوَلَّوا۟ وَّأَعْيُنُهُمْ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمْعِ حَزَنًا أَلَّا يَجِدُوا۟ مَا يُنفِقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala wale wanaokujia ili uwape kipando, ukasema: Sina kipando cha kukubebeeni juu yake, kwa hivyo wanageuka kwenda huku macho yao yanamiminika machozi kwa huzuni ya kwamba hawatapata cha kutoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّمَا ٱلسَّبِيلُ عَلَى ٱلَّذِينَ يَسْتَـْٔذِنُونَكَ وَهُمْ أَغْنِيَآءُ رَضُوا۟ بِأَن يَكُونُوا۟ مَعَ ٱلْخَوَالِفِ وَطَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika njia ya lawama iko tu juu ya wale wanaokuomba ruhusa wasiende vitani ilhali wao ni matajiri. Waliridhia kwamba wawe pamoja na wanaosalia nyuma. Na Mwenyezi Mungu akaiziba mioyo yao. Kwa hivyo hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْتَذِرُونَ إِلَيْكُمْ إِذَا رَجَعْتُمْ إِلَيْهِمْ قُل لَّا تَعْتَذِرُوا۟ لَن نُّؤْمِنَ لَكُمْ قَدْ نَبَّأَنَا ٱللَّهُ مِنْ أَخْبَارِكُمْ وَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُۥ ثُمَّ تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatawatolea udhuru mtakapowarudia. Sema: Msitoe udhuru; hatutawaamini. Mwenyezi Mungu amekwishatujulisha habari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhahiri; naye atawaambia mliyokuwa mkiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَيَحْلِفُونَ بِٱللَّهِ لَكُمْ إِذَا ٱنقَلَبْتُمْ إِلَيْهِمْ لِتُعْرِضُوا۟ عَنْهُمْ فَأَعْرِضُوا۟ عَنْهُمْ إِنَّهُمْ رِجْسٌ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatawaapia kwa Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili muwaachilie mbali. Basi waachilieni mbali. Hakika hao ni najisi, na makazi yao ni Jahannam, kuwa ni malipo kwa yale waliyokuwa wakiyachuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَحْلِفُونَ لَكُمْ لِتَرْضَوْا۟ عَنْهُمْ فَإِن تَرْضَوْا۟ عَنْهُمْ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَرْضَىٰ عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْفَٰسِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanawaapia ili muwe radhi nao. Lakini hata mkiwa radhi nao nyiye, basi hakika Mwenyezi Mungu hawi radhi na kaumu wavukao mipaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْأَعْرَابُ أَشَدُّ كُفْرًا وَنِفَاقًا وَأَجْدَرُ أَلَّا يَعْلَمُوا۟ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMabedui ndio wenye ukafiri mkubwa zaidi na unafiki, na wameelekea zaidi kutojua mipaka ya yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu juu ya Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنَ ٱلْأَعْرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغْرَمًا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَ عَلَيْهِمْ دَآئِرَةُ ٱلسَّوْءِ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Mabedui hao kuna yule anayefikiri kuwa kile anachotoa ni gharama ya bure, na anakutazamieni mambo yawageukie. Mageuko maovu yatakuwa juu yao! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنَ ٱلْأَعْرَابِ مَن يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِ أَلَآ إِنَّهَا قُرْبَةٌ لَّهُمْ سَيُدْخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِى رَحْمَتِهِۦٓ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Mabedui kuna yule anayemwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na anakichukulia kile anachotoa kuwa ni cha kumsongeza karibu na Mwenyezi Mungu na cha kupata kwacho dua za Mtume. Ndiyo! Hayo hakika ni mambo ya kuwasongeza karibu. Mwenyezi Mungu atawaingiza katika rehema yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلْأَوَّلُونَ مِنَ ٱلْمُهَٰجِرِينَ وَٱلْأَنصَارِ وَٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُم بِإِحْسَٰنٍ رَّضِىَ ٱللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا۟ عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّٰتٍ تَجْرِى تَحْتَهَا ٱلْأَنْهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًا ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliotangulia, wa kwanza, katika Wahajiri na Ansari, na wale waliowafuata kwa uzuri, Mwenyezi Mungu aliwaridhia, na wao walimridhia, na amewaandalia Bustani zipitazo mito chini yake, watadumu humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِمَّنْ حَوْلَكُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ مُنَٰفِقُونَ وَمِنْ أَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ مَرَدُوا۟ عَلَى ٱلنِّفَاقِ لَا تَعْلَمُهُمْ نَحْنُ نَعْلَمُهُمْ سَنُعَذِّبُهُم مَّرَّتَيْنِ ثُمَّ يُرَدُّونَ إِلَىٰ عَذَابٍ عَظِيمٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika mabedui walio jirani zenu kuna wanafiki; na katika wakazi wa Madina pia wapo wale waliobobea katika unafiki. Wewe huwajui. Sisi tunawajua. Tutawaadhibu mara mbili, kisha watarudishwa kwenye adhabu kubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاخَرُونَ ٱعْتَرَفُوا۟ بِذُنُوبِهِمْ خَلَطُوا۟ عَمَلًا صَٰلِحًا وَءَاخَرَ سَيِّئًا عَسَى ٱللَّهُ أَن يَتُوبَ عَلَيْهِمْ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wengine walikiri dhambi zao, walichanganya matendo mema na mengine mabaya. Huenda Mwenyezi Mungu akakubali toba zao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

خُذْ مِنْ أَمْوَٰلِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ إِنَّ صَلَوٰتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterChukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwayo, na waombee dua. Hakika kuomba dua kwako ni utulivu kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ يَعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقْبَلُ ٱلتَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِۦ وَيَأْخُذُ ٱلصَّدَقَٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anakubali toba ya waja wake, na anazichukua sadaka, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba, Mwenye kurehemu sana?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقُلِ ٱعْمَلُوا۟ فَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمْ وَرَسُولُهُۥ وَٱلْمُؤْمِنُونَ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sema: Tendeni matendo. Na Mwenyezi Mungu atayaona matendo yenu, na Mtume wake, na Waumini. Na mtarudishwa kwa Mwenye kujua siri na dhahiri; basi naye atawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَءَاخَرُونَ مُرْجَوْنَ لِأَمْرِ ٱللَّهِ إِمَّا يُعَذِّبُهُمْ وَإِمَّا يَتُوبُ عَلَيْهِمْ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wapo wengine wanaongojea amri ya Mwenyezi Mungu. Ima atawaadhibu au atawakubalia toba. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua zaidi, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُوا۟ مَسْجِدًا ضِرَارًا وَكُفْرًا وَتَفْرِيقًۢا بَيْنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَإِرْصَادًا لِّمَنْ حَارَبَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ مِن قَبْلُ وَلَيَحْلِفُنَّ إِنْ أَرَدْنَآ إِلَّا ٱلْحُسْنَىٰ وَٱللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَٰذِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wapo waliojenga msikiti kwa ajili ya madhara, na ukafiri, na kuwafarikisha Waumini, na pa kuvizia kwa ajili ya wale waliompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake hapo kabla. Na bila ya shaka wataapa kwamba: 'Hatukukusudia isipokuwa uzuri tu.' Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa wao hakika ni waongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا تَقُمْ فِيهِ أَبَدًا لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى ٱلتَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا۟ وَٱللَّهُ يُحِبُّ ٱلْمُطَّهِّرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUsisimame ndani yake kabisa. Msikiti uliojengwa juu ya msingi wa ucha Mungu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo wanaume wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanaojitakasa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَٰنَهُۥ عَلَىٰ تَقْوَىٰ مِنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنٍ خَيْرٌ أَم مَّنْ أَسَّسَ بُنْيَٰنَهُۥ عَلَىٰ شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَٱنْهَارَ بِهِۦ فِى نَارِ جَهَنَّمَ وَٱللَّهُ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya uchaji utokao kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora zaidi au mwenye kuweka msingi wa mjengo wake juu ya ukingo wa shimo unaoporomoka? Kwa hivyo ukaporomoka naye ndani ya Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu madhalimu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا يَزَالُ بُنْيَٰنُهُمُ ٱلَّذِى بَنَوْا۟ رِيبَةً فِى قُلُوبِهِمْ إِلَّآ أَن تَقَطَّعَ قُلُوبُهُمْ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mjengo wao huo walioujenga hautaacha kuwa shaka katika nyoyo zao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ ٱشْتَرَىٰ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَٰلَهُم بِأَنَّ لَهُمُ ٱلْجَنَّةَ يُقَٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِى ٱلتَّوْرَىٰةِ وَٱلْإِنجِيلِ وَٱلْقُرْءَانِ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِۦ مِنَ ٱللَّهِ فَٱسْتَبْشِرُوا۟ بِبَيْعِكُمُ ٱلَّذِى بَايَعْتُم بِهِۦ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu alinunua kutoka kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao wana Bustani ya mbinguni. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo wanaua na wanauawa. Hii ni ahadi aliyojilazimisha (Mwenyezi Mungu) kwa haki katika Taurati, na Injili, na Qur-ani. Na nani atimizaye zaidi ahadi yake zaidi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyofanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلتَّٰٓئِبُونَ ٱلْعَٰبِدُونَ ٱلْحَٰمِدُونَ ٱلسَّٰٓئِحُونَ ٱلرَّٰكِعُونَ ٱلسَّٰجِدُونَ ٱلْـَٔامِرُونَ بِٱلْمَعْرُوفِ وَٱلنَّاهُونَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَٱلْحَٰفِظُونَ لِحُدُودِ ٱللَّهِ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wanaotubia, wanaoabudu, wanaohimidi, wanaokimbilia heri, wanaorukuu, wanaosujudu, wanaoamrisha mema na wanaokataza maovu, na wanaolinda mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na wabashirie Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا كَانَ لِلنَّبِىِّ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن يَسْتَغْفِرُوا۟ لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوٓا۟ أُو۟لِى قُرْبَىٰ مِنۢ بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُمْ أَصْحَٰبُ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaimpasii Nabii na wale walioamini kuwaombea msamaha washirikina, hata wakiwa ni jamaa zao, baada ya kwishawabainikia kuwa hao ni watu wa Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ ٱسْتِغْفَارُ إِبْرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَآ إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُۥٓ أَنَّهُۥ عَدُوٌّ لِّلَّهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ إِنَّ إِبْرَٰهِيمَ لَأَوَّٰهٌ حَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala haikuwa Ibrahim kumtakia msamaha baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyomuahidi. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui ya Mwenyezi Mungu, alijiweka mbali mno naye. Hakika Ibrahim alikuwa mwingi wa kuomba, mnyenyekevu, mvumilivu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُضِلَّ قَوْمًۢا بَعْدَ إِذْ هَدَىٰهُمْ حَتَّىٰ يُبَيِّنَ لَهُم مَّا يَتَّقُونَ إِنَّ ٱللَّهَ بِكُلِّ شَىْءٍ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwapotosha kaumu baada ya kwishawaongoa mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua vyema kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ يُحْىِۦ وَيُمِيتُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا نَصِيرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu zote na ardhi; huhuisha na hufisha. Nanyi hamna mlinzi yeyote wala msaidizi kando na Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِىِّ وَٱلْمُهَٰجِرِينَ وَٱلْأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِى سَاعَةِ ٱلْعُسْرَةِ مِنۢ بَعْدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٍ مِّنْهُمْ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ إِنَّهُۥ بِهِمْ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu alikwishakubali toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari waliomfuata katika saa ya ugumu, baada ya kwamba nyoyo za kundi miongoni mwao zilikuwa zimekaribia kukengeuka. Basi akakubali toba yao. Hakika Yeye kwao ni Mpole, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُوا۟ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ ٱلْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوٓا۟ أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pia wale watatu walioachwa nyuma hata ardhi wakaiona kuwa ni finyu juu yao, pamoja na ukunjufu wake, na nafsi zao zikawabana, na wakayakinika kuwa hakuna kimbilio kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake Yeye. Kisha akawakubalia toba ili nao watubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukubali toba sana, Mwenye kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَكُونُوا۟ مَعَ ٱلصَّٰدِقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا كَانَ لِأَهْلِ ٱلْمَدِينَةِ وَمَنْ حَوْلَهُم مِّنَ ٱلْأَعْرَابِ أَن يَتَخَلَّفُوا۟ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرْغَبُوا۟ بِأَنفُسِهِمْ عَن نَّفْسِهِۦ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ لَا يُصِيبُهُمْ ظَمَأٌ وَلَا نَصَبٌ وَلَا مَخْمَصَةٌ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوْطِئًا يَغِيظُ ٱلْكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنْ عَدُوٍّ نَّيْلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٌ صَٰلِحٌ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ ٱلْمُحْسِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaiwafailii watu wa Madina na Mabedui walio kando kando yao kusalia nyuma wasitoke pamoja na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko nafsi yake. Hayo ni kwa sababu wao hakiwapati kiu, wala machovu, wala njaa, katika Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaendi mahali panapowaghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, isipokuwa huandikiwa kwa hicho kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanaofanya uzuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَا يُنفِقُونَ نَفَقَةً صَغِيرَةً وَلَا كَبِيرَةً وَلَا يَقْطَعُونَ وَادِيًا إِلَّا كُتِبَ لَهُمْ لِيَجْزِيَهُمُ ٱللَّهُ أَحْسَنَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hawatoi masurufu madogo wala makubwa, wala hawalivuki bonde, isipokuwa huandikiwa, ili Mwenyezi Mungu awalipe bora zaidi ya yale waliyokuwa wakiyatenda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا كَانَ ٱلْمُؤْمِنُونَ لِيَنفِرُوا۟ كَآفَّةً فَلَوْلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرْقَةٍ مِّنْهُمْ طَآئِفَةٌ لِّيَتَفَقَّهُوا۟ فِى ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُوا۟ قَوْمَهُمْ إِذَا رَجَعُوٓا۟ إِلَيْهِمْ لَعَلَّهُمْ يَحْذَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa haiwapasi Waumini kutoka wote pamoja. Lakini kwa nini hawatoki baadhi katika kila kundi miongoni mwao, wakajifunze vyema Dini, na kisha waje kuwaonya wenzao watakapowarudia, ili wajihadharishe?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ قَٰتِلُوا۟ ٱلَّذِينَ يَلُونَكُم مِّنَ ٱلْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا۟ فِيكُمْ غِلْظَةً وَٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُتَّقِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi mlioamini! Piganeni na wale walio karibu yenu miongoni mwa makafiri, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ فَمِنْهُم مَّن يَقُولُ أَيُّكُمْ زَادَتْهُ هَٰذِهِۦٓ إِيمَٰنًا فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فَزَادَتْهُمْ إِيمَٰنًا وَهُمْ يَسْتَبْشِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa inapokwishateremshwa sura, basi wapo miongoni mwao wasemao: "Ni nani miongoni mwenu sura hii imemzidishia Imani?" Ama wale walioamini, iliwazidishia Imani, nao wanafurahi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَتْهُمْ رِجْسًا إِلَىٰ رِجْسِهِمْ وَمَاتُوا۟ وَهُمْ كَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ama wale wenye maradhi katika nyoyo zao, basi iliwazidishia uovu juu ya uovu wao; na wanakufa hali ya kuwa wao ni makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَا يَرَوْنَ أَنَّهُمْ يُفْتَنُونَ فِى كُلِّ عَامٍ مَّرَّةً أَوْ مَرَّتَيْنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمْ يَذَّكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaoni ya kwamba wanajaribiwa kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا مَآ أُنزِلَتْ سُورَةٌ نَّظَرَ بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ هَلْ يَرَىٰكُم مِّنْ أَحَدٍ ثُمَّ ٱنصَرَفُوا۟ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikishateremka sura, hutazamana wao kwa wao, (kama kwamba wanasema:) "Je, yuko yeyote anayewaona nyinyi" Kisha huondoka wakaenda. Mwenyezi akaziondoa nyoyo zao kwa kuwa hao ni kaumu wasiofahamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَقَدْ جَآءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِٱلْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika amekwishawajia Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yale yanayowataabisha, anawajali sana, kwa Waumini ni mpole na mwenye kuwarehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِن تَوَلَّوْا۟ فَقُلْ حَسْبِىَ ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ ٱلْعَرْشِ ٱلْعَظِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hivyo, wakigeuka, basi wewe sema, ”Mwenyezi Mungu ananitosha. Hakuna mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi ninamtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70