وَإِذَا مَسَّ ٱلْإِنسَٰنَ ٱلضُّرُّ دَعَانَا لِجَنۢبِهِۦٓ أَوْ قَاعِدًا أَوْ قَآئِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُۥ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَآ إِلَىٰ ضُرٍّ مَّسَّهُۥ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mtu akiguswa na shida, hutuomba naye ameegesha ubavu, au amekaa au amesimama. Lakini tunapomwondoshea shida yake hiyo, huendelea kama kwamba hakuwahi kutuomba tumwondoshee shida iliyomgusa. Hivyo ndivyo walivyopambiwa wapitilizao viwango yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa mtu akiguswa na shida hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama. Lakini tukimwondoshea shida yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba tumwondoshee shida iliyo mpata. Ndio namna hiyo wamepambiwa warukao mipaka yale waliyo kuwa wakiyatenda.