وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّءَا لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ بُيُوتًا وَٱجْعَلُوا۟ بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukamteremshia ufunuo (wahyi) Musa na ndugu yake kuwa: Watengenezeeni majumba kaumu yenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndimo mahali pa ibada, na mdumishe Swala, na wape habari njema Waumini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tukampelekea Musa na ndugu yake wahyi huu: Watengenezeeni majumba watu wenu katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndio mwahali mwa ibada, na mshike Swala, na wabashirie Waumini.