وَيَقُولُونَ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ فَقُلْ إِنَّمَا ٱلْغَيْبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓا۟ إِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُنتَظِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanasema, “Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?” Sema, “Hakika mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu tu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi niko pamoja nanyi katika wanaongojea.”
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wanasema: Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi ni pamoja nanyi katika wanao ngojea.