وَمَا كَانَ ٱلنَّاسُ إِلَّآ أُمَّةً وَٰحِدَةً فَٱخْتَلَفُوا۟ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِىَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu hawakuwa isipokuwa Umma mmoja tu, kisha wakahitilafiana. Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi, hakuna shaka hukumu ingelikwishakatwa baina yao katika yale wanayohitilafiana.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si neno lililo kwisha tangulia kutokana na Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana.