Mwanzo › Sura › Sura Al-Muddaththir
Sura Al-Muddaththir المدثر
Aya 56 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 4
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يَٰٓأَيُّهَا ٱلْمُدَّثِّرُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe uliyejigubika!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُمْ فَأَنذِرْ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Simama uonye!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Mola wako Mlezi mtukuze!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na nguo zako, zisafishe.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلرُّجْزَ فَٱهْجُرْ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na yaliyo machafu yahame!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلِرَبِّكَ فَٱصْبِرْ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَإِذَا نُقِرَ فِى ٱلنَّاقُورِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi litakapopulizwa baragumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَلَى ٱلْكَٰفِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ذَرْنِى وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Niache peke yangu na niliyemuumba.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَعَلْتُ لَهُۥ مَالًا مَّمْدُودًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na nikamjaalia awe na mali mengi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَبَنِينَ شُهُودًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na wana wanaoonekana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَهَّدتُّ لَهُۥ تَمْهِيدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na nikamtegenezea mambo vizuri kabisa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha anatumai nimzidishie!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّهُۥ كَانَ لِـَٔايَٰتِنَا عَنِيدًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia ukaidi Aya zetu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
سَأُرْهِقُهُۥ صَعُودًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nitamtesa kwa mateso yasiowezekana.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّهُۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ameangamia! Vipi alivyopima!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Tena ameangamia! Vipi alivyopima!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ نَظَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha akatazama.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ثُمَّ أَدْبَرَ وَٱسْتَكْبَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَقَالَ إِنْ هَٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulionukuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنْ هَٰذَآ إِلَّا قَوْلُ ٱلْبَشَرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Haya si chochote ila kauli ya binadamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
سَأُصْلِيهِ سَقَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سَقَرُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَا تُبْقِى وَلَا تَذَرُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Haubakishi wala hausazi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Unababua ngozi iwe nyeusi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Juu yake wapo kumi na tisa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا جَعَلْنَآ أَصْحَٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَٰٓئِكَةً وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِيَسْتَيْقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ وَيَزْدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِيمَٰنًا وَلَا يَرْتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَٰبَ وَٱلْمُؤْمِنُونَ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْكَٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَٰذَا مَثَلًا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ وَمَا هِىَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha waliokufuru, wapate kuwa na yakini waliopewa Kitabu, na wazidi Imani wale walioamini, wala wasiwe na shaka waliopewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: "Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu?" Ndiyo kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anayejua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binadamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّا وَٱلْقَمَرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hasha! Naapa kwa mwezi!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa usiku unapokucha!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلصُّبْحِ إِذَآ أَسْفَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa asubuhi inapopambazuka!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّهَا لَإِحْدَى ٱلْكُبَرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ni onyo kwa binaadamu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
لِمَن شَآءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa anayetaka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كُلُّ نَفْسٍۭ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyoyachuma.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِلَّآ أَصْحَٰبَ ٱلْيَمِينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Isipokuwa watu wa kuliani.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فِى جَنَّٰتٍ يَتَسَآءَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
Tazama tafsiri zote za aya hii →
عَنِ ٱلْمُجْرِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Habari za wakosefu:
Tazama tafsiri zote za aya hii →
مَا سَلَكَكُمْ فِى سَقَرَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ni nini kilichokupelekeni Motoni?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قَالُوا۟ لَمْ نَكُ مِنَ ٱلْمُصَلِّينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Waseme: Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ ٱلْمِسْكِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلْخَآئِضِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tulikuwa tukizama pamoja na waliozama katika maovu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na tulikuwa tukiikanusha Siku ya Malipo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلْيَقِينُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mpaka yakini (yaani mauti) ilipotufikia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَٰعَةُ ٱلشَّٰفِعِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَا لَهُمْ عَنِ ٱلتَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kana kwamba wao ni mapunda waliotimuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍۭ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wanaomkimbia simba!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
بَلْ يُرِيدُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizofunuliwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّا بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِنَّهُۥ تَذْكِرَةٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi anayetaka atakumbuka.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ هُوَ أَهْلُ ٱلتَّقْوَىٰ وَأَهْلُ ٱلْمَغْفِرَةِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na hawatakumbuka isipokuwa Mwenyezi Mungu atake. Ucha Mungu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Muzzammil
Sura Al-Qiyaama →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.