Mwanzo › Sura › Sura Al-Muzzammil
Sura Al-Muzzammil المزمل
Aya 20 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 3
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ يَٰٓأَيُّهَا ٱلْمُزَّمِّلُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe uliyejifunika!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
قُمِ ٱلَّيْلَ إِلَّا قَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kesha usiku kucha, ila kidogo tu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
نِّصْفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصْ مِنْهُ قَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Nusu yake, au ipunguze kidogo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَوْ زِدْ عَلَيْهِ وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Au izidishe - na soma Qur-ani kwa utaratibu na utungo.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّا سَنُلْقِى عَلَيْكَ قَوْلًا ثَقِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tutakuteremshia kauli nzito.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيْلِ هِىَ أَشَدُّ وَطْـًٔا وَأَقْوَمُ قِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika kuamka usiku kunawafikiana zaidi na moyo, na maneno yake yanatua zaidi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ لَكَ فِى ٱلنَّهَارِ سَبْحًا طَوِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani hakika mchana una shughuli nyingi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱذْكُرِ ٱسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
رَّبُّ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذْهُ وَكِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Mola Mlezi wa mashariki na magharibi, hapana mungu isipokuwa Yeye, basi mfanye kuwa Mtegemewa wako.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهْجُرْهُمْ هَجْرًا جَمِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na vumilia hayo wayasemayo, na jitenge nao kwa vizuri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَذَرْنِى وَٱلْمُكَذِّبِينَ أُو۟لِى ٱلنَّعْمَةِ وَمَهِّلْهُمْ قَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na niache Mimi na hao wanaokanusha, walioneemeka; na wape muhula kidogo!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ لَدَيْنَآ أَنكَالًا وَجَحِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tunazo pingu nzito na Moto unaowaka kwa ukali kabisa!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَطَعَامًا ذَا غُصَّةٍ وَعَذَابًا أَلِيمًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na chakula kinachokwama kooni, na adhabu inayoumiza.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَوْمَ تَرْجُفُ ٱلْأَرْضُ وَٱلْجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلْجِبَالُ كَثِيبًا مَّهِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Siku ambayo ardhi itatikiswa na milima pia, na milima itakuwa kama tifutifu la mchanga!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّآ أَرْسَلْنَآ إِلَيْكُمْ رَسُولًا شَٰهِدًا عَلَيْكُمْ كَمَآ أَرْسَلْنَآ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ رَسُولًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Sisi tumemtuma kwenu Mtume aliye shahidi juu yenu, kama tulivyomtuma Mtume kwa Firauni.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَعَصَىٰ فِرْعَوْنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذْنَٰهُ أَخْذًا وَبِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Lakini Firauni alimuasi huyo Mtume, basi tukamshika mshiko wa mateso.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَكَيْفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرْتُمْ يَوْمًا يَجْعَلُ ٱلْوِلْدَٰنَ شِيبًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرٌۢ بِهِۦ كَانَ وَعْدُهُۥ مَفْعُولًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hapo mbingu zitapasuka kwa sababu yake! Ahadi yake itakuwa imetekelezwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذْكِرَةٌ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwa hakika hili ni kumbusho. Mwenye kutaka atashika Njia ya kwendea kwa Mola wake Mlezi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ رَبَّكَ يَعْلَمُ أَنَّكَ تَقُومُ أَدْنَىٰ مِن ثُلُثَىِ ٱلَّيْلِ وَنِصْفَهُۥ وَثُلُثَهُۥ وَطَآئِفَةٌ مِّنَ ٱلَّذِينَ مَعَكَ وَٱللَّهُ يُقَدِّرُ ٱلَّيْلَ وَٱلنَّهَارَ عَلِمَ أَن لَّن تُحْصُوهُ فَتَابَ عَلَيْكُمْ فَٱقْرَءُوا۟ مَا تَيَسَّرَ مِنَ ٱلْقُرْءَانِ عَلِمَ أَن سَيَكُونُ مِنكُم مَّرْضَىٰ وَءَاخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِى ٱلْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ ٱللَّهِ وَءَاخَرُونَ يُقَٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَٱقْرَءُوا۟ مَا تَيَسَّرَ مِنْهُ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُوا۟ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَقْرِضُوا۟ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا وَمَا تُقَدِّمُوا۟ لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ ٱللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا وَٱسْتَغْفِرُوا۟ ٱللَّهَ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌۢ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Mola wako Mlezi anajua ya kuwa hakika wewe unakesha karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake, na thuluthi yake. Na baadhi ya watu walio pamoja nawe kadhalika. Na Mwenyezi Mungu ndiye anayeukadiria usiku na mchana. Anajua kuwa hamwezi kuweka hisabu, basi amekusameheni. Basi someni kilicho chepesi katika Qur-ani. Anajua ya kuwa baadhi yenu watakuwa wagonjwa, na wengine wanasafiri katika ardhi wakitafuta fadhila ya Mwenyezi Mungu, na wengine wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo someni kilicho chepesi humo, na mshike Sala, na toeni Zaka, na mkopesheni Mwenyezi Mungu mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana. Na mtakeni msamaha Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Jinn
Sura Al-Muddaththir →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.