ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِى سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ ٱلرَّحْمَٰنُ فَسْـَٔلْ بِهِۦ خَبِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye aliziumba mbingu na ardhi, na vilivyo kati yake kwa siku sita. Kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi. Mwingi wa rehema (Arrahman)! Uliza habari zake kwa amjuaye.[1]
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa wamjuaye.