caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ar-Room الروم

Aya 60 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 84

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ الٓمٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlif Lam Mim.[1]

Tazama tafsiri zote za aya hii →

غُلِبَتِ ٱلرُّومُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWarumi wameshindwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِىٓ أَدْنَى ٱلْأَرْضِ وَهُم مِّنۢ بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى بِضْعِ سِنِينَ لِلَّهِ ٱلْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِنۢ بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ ٱلْمُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika miaka michache. Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بِنَصْرِ ٱللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَآءُ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwingi wa kurehemu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَعْدَ ٱللَّهِ لَا يُخْلِفُ ٱللَّهُ وَعْدَهُۥ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu havunji ahadi yake. Lakini wengi wa watu hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْلَمُونَ ظَٰهِرًا مِّنَ ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ ٱلْـَٔاخِرَةِ هُمْ غَٰفِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanajua hali ya dhahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا۟ فِىٓ أَنفُسِهِم مَّا خَلَقَ ٱللَّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ ٱلنَّاسِ بِلِقَآئِ رَبِّهِمْ لَكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yake isipokuwa kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukufuru kuwa watakutana na Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَانُوٓا۟ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا۟ ٱلْأَرْضَ وَعَمَرُوهَآ أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawatembei katika ardhi wakaona ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Nao walikuwa na nguvu zaidi kuliko wao, na wakaitimbua ardhi na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha wao. Na Mitume wao wakawajia na ushahidi wa wazi. Basi hakuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye kuwadhulumu, lakini wenyewe walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ كَانَ عَٰقِبَةَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔوا۟ ٱلسُّوٓأَىٰٓ أَن كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَكَانُوا۟ بِهَا يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha ulikuwa mwisho wa wale waliofanya ubaya ni mbaya zaidi kwa sababu walizikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na wakawa wanazifanyia stihizai.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu huanzisha uumbaji, tena akaurudisha mara ya pili, na kisha mtarejeshwa kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُبْلِسُ ٱلْمُجْرِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku itakaposimama Saa ya Kiyama, wahalifu watakata tamaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَآئِهِمْ شُفَعَٰٓؤُا۟ وَكَانُوا۟ بِشُرَكَآئِهِمْ كَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala hawatakuwa na waombezi wowote miongoni mwa wale waliokuwa wakiwashirikisha na Mwenyezi Mungu; na wao wenyewe watawakataa hao washirikishwa wao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku itakaposimama Saa ya Kiyama, siku hiyo watatengana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَهُمْ فِى رَوْضَةٍ يُحْبَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma wale walioamini na wakatenda mema, watafurahishwa katika Bustani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَمَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِنَا وَلِقَآئِ ٱلْـَٔاخِرَةِ فَأُو۟لَٰٓئِكَ فِى ٱلْعَذَابِ مُحْضَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ama wale waliokufuru na wakazikanusha Ishara zetu na mkutano wa Akhera, hao basi watahudhurishwa katika adhabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسُبْحَٰنَ ٱللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Subhanallah (Mtakaseni Mwenyezi Mungu) jioni na asubuhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَهُ ٱلْحَمْدُ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يُخْرِجُ ٱلْحَىَّ مِنَ ٱلْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ ٱلْمَيِّتَ مِنَ ٱلْحَىِّ وَيُحْىِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHukitoa kilicho hai kutokana na kilichokufa, na hukitoa kilichokufa kutokana na kilicho hai. Na huihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Na kama hivyo ndivyo mtavyofufuliwa."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَآ أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kuwa aliwaumba kwa udongo. Kisha mmekuwa watu mliotawanyika kote kote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَٰجًا لِّتَسْكُنُوٓا۟ إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kuwa aliwaumbia wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye ameweka mapenzi na rehema baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaotafakari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦ خَلْقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱخْتِلَٰفُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَٰنِكُمْ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّلْعَٰلِمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutofautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦ مَنَامُكُم بِٱلَّيْلِ وَٱلنَّهَارِ وَٱبْتِغَآؤُكُم مِّن فَضْلِهِۦٓ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kulala kwenu usiku na mchana, na kutafuta kwenu fadhila zake. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanaosikia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦ يُرِيكُمُ ٱلْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَيُحْىِۦ بِهِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَآ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake huwaonyesha umeme kwa kuwatia hofu na tamaa. Na huwateremshia maji kutoka mbinguni, na kwa hayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu watumiao akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَن تَقُومَ ٱلسَّمَآءُ وَٱلْأَرْضُ بِأَمْرِهِۦ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ ٱلْأَرْضِ إِذَآ أَنتُمْ تَخْرُجُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kuwa mbingu na ardhi zimesimama kwa amri yake. Kisha atakapowaita mwito mmoja tu, hapo mtatoka kwenye ardhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ كُلٌّ لَّهُۥ قَٰنِتُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamtii Yeye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِى يَبْدَؤُا۟ ٱلْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُۥ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ وَلَهُ ٱلْمَثَلُ ٱلْأَعْلَىٰ فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Yeye ndiye anayeanzisha uumbaji, kisha ataurudisha mara nyingine. Na jambo hili ni jepesi zaidi kwake. Naye ndiye mwenye mfano bora zaidi katika mbingu na ardhi. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَٰنُكُم مِّن شُرَكَآءَ فِى مَا رَزَقْنَٰكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَآءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَٰتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu watumiao akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلِ ٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ أَهْوَآءَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ فَمَن يَهْدِى مَنْ أَضَلَّ ٱللَّهُ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali waliodhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi ni nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِى فَطَرَ ٱلنَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ ٱللَّهِ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini kwa unyoofu, ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَٱتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَلَا تَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMuwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na simamisheni Swala, na wala msiwe katika washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِنَ ٱلَّذِينَ فَرَّقُوا۟ دِينَهُمْ وَكَانُوا۟ شِيَعًا كُلُّ حِزْبٍۭ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَا مَسَّ ٱلنَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا۟ رَبَّهُم مُّنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَآ أَذَاقَهُم مِّنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watu wanapoguswa na madhara, humwomba Mola wao Mlezi huku wanatubu kwake. Kisha akiwaonjesha rehema itokayo kwake, mara kikundi miongoni mwao humshirikisha Mola wao Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيَكْفُرُوا۟ بِمَآ ءَاتَيْنَٰهُمْ فَتَمَتَّعُوا۟ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa kuyakufuru yale tuliyowapa. Basi stareheni. Mtakuja jua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَٰنًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا۟ بِهِۦ يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAu tumewateremshia hoja ambayo inazungumza juu ya kile walichokuwa wakishirikisha nacho?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذَآ أَذَقْنَا ٱلنَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا۟ بِهَا وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌۢ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tunapowaonjesha watu rehema, huifurahia. Na ukiwasibu ubaya kwa iliyoyatanguliza mikono yao wenyewe, mara wanakata tamaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّ ٱللَّهَ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia amtakaye? Hakika katika hayo, zipo Ishara kwa watu wanaoamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَـَٔاتِ ذَا ٱلْقُرْبَىٰ حَقَّهُۥ وَٱلْمِسْكِينَ وَٱبْنَ ٱلسَّبِيلِ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ ٱللَّهِ وَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mpe jamaa haki yake, na masikini, na msafiri. Hayo ni heri kwa wanaotaka uso wa Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waliofaulu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ ءَاتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَا۟ فِىٓ أَمْوَٰلِ ٱلنَّاسِ فَلَا يَرْبُوا۟ عِندَ ٱللَّهِ وَمَآ ءَاتَيْتُم مِّن زَكَوٰةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ ٱللَّهِ فَأُو۟لَٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُضْعِفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka uso wa Mwenyezi Mungu, basi hao ndio watakaozidishiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ هَلْ مِن شُرَكَآئِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَىْءٍ سُبْحَٰنَهُۥ وَتَعَٰلَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba, kisha akawaruzuku, kisha atawafisha, na kisha atawafufua. Je, yupo yeyote katika hao mnaowashirikisha na Mwenyezi Mungu afanyae lolote katika hayo? Yeye ametakasika, na ametukuka mbali na hayo mnayomshirikisha naye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ظَهَرَ ٱلْفَسَادُ فِى ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ ٱلَّذِى عَمِلُوا۟ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUharibifu umedhihiri barani na baharini kwa yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonjeshe baadhi ya yale waliyoyatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ سِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَٱنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلُ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Safirini duniani na muangalie ulikuwaje mwisho wa wale waliotangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ ٱلْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُۥ مِنَ ٱللَّهِ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini iliyonyooka kabla ya kufika Siku hiyo isiyozuilika, inayotoka kwa Mwenyezi Mungu. Siku hiyo watu watatengana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُۥ وَمَنْ عَمِلَ صَٰلِحًا فَلِأَنفُسِهِمْ يَمْهَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayekufuru, basi ukafiri wake utakuwa juu yake mwenyewe. Na anayetenda mema, basi wanazitengenezea nafsi zao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِيَجْزِىَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن فَضْلِهِۦٓ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIli awalipe wale walioamini na wakatenda mema kutokana na fadhila yake. Hakika Yeye hawapendi makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَن يُرْسِلَ ٱلرِّيَاحَ مُبَشِّرَٰتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحْمَتِهِۦ وَلِتَجْرِىَ ٱلْفُلْكُ بِأَمْرِهِۦ وَلِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili kuwaonjesha baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yaende kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَآءُوهُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ فَٱنتَقَمْنَا مِنَ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ ٱلْمُؤْمِنِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulikwishawatuma Mitume kabla yako kwa kaumu zao, na wakawajia kwa hoja zilizo wazi. Tukawaadhibu wale waliofanya uhalifu. Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى يُرْسِلُ ٱلرِّيَٰحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُۥ فِى ٱلسَّمَآءِ كَيْفَ يَشَآءُ وَيَجْعَلُهُۥ كِسَفًا فَتَرَى ٱلْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَٰلِهِۦ فَإِذَآ أَصَابَ بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦٓ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye anayezituma pepo zikayatimua mawingu, kisha akayatandaza mbinguni kama apendavyo. Na akayafanya mapande mapande, basi ukaiona mvua inatoka ndani yake. Anapowafikishia awatakao katika waja wake, mara hao huwa na furaha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن كَانُوا۟ مِن قَبْلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْهِم مِّن قَبْلِهِۦ لَمُبْلِسِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ingawa kabla ya kuteremshiwa walikuwa wenye kukata tamaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱنظُرْ إِلَىٰٓ ءَاثَٰرِ رَحْمَتِ ٱللَّهِ كَيْفَ يُحْىِ ٱلْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَآ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْىِ ٱلْمَوْتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi ziangalie athari za rehema ya Mwenyezi Mungu, jinsi anavyoihuisha ardhi baada ya kufa kwake. Basi hakika huyo ndiye bila ya shaka mwenye kuhuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَّظَلُّوا۟ مِنۢ بَعْدِهِۦ يَكْفُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tungeutuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya manjano, juu ya hayo wangeendelea kukufuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ ٱلْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ ٱلصُّمَّ ٱلدُّعَآءَ إِذَا وَلَّوْا۟ مُدْبِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala viziwi wakasikia wito wakishageuka kukupa mgongo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَآ أَنتَ بِهَٰدِ ٱلْعُمْىِ عَن ضَلَٰلَتِهِمْ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِـَٔايَٰتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala wewe huwaongoi vipofu kutoka katika upotovu wao. Huwasikilizishi isipokuwa wale wanaoziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walionyenyekea.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِنۢ بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً يَخْلُقُ مَا يَشَآءُ وَهُوَ ٱلْعَلِيمُ ٱلْقَدِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye aliyewaumba kutokana na udhaifu, kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye ajuaye zaidi, Mwenye uweza wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ يُقْسِمُ ٱلْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا۟ غَيْرَ سَاعَةٍ كَذَٰلِكَ كَانُوا۟ يُؤْفَكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa siku itakaposimama Saa ya Kiyama, wahalifu wataapa kwamba hawakukaa duniani isipokuwa saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakipotoshwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ وَٱلْإِيمَٰنَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِى كِتَٰبِ ٱللَّهِ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْبَعْثِ فَهَٰذَا يَوْمُ ٱلْبَعْثِ وَلَٰكِنَّكُمْ كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliopewa elimu na Imani watasema: Hakika nyinyi mlikwishakaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَيَوْمَئِذٍ لَّا يَنفَعُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Siku hiyo hautawafaa wale waliodhulumu udhuru wao, wala haitatakiwa toba yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِى هَٰذَا ٱلْقُرْءَانِ مِن كُلِّ مَثَلٍ وَلَئِن جِئْتَهُم بِـَٔايَةٍ لَّيَقُولَنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُبْطِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii Qur-ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote, hapana shaka wale waliokufuru watasema, "Nyinyi si chochote isipokuwa ni wana batili."

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za wale wasiojua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ ٱلَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Wala kamwe wasikupaparishe hao wasiokuwa na yakini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70