وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦٓ أَن يُرْسِلَ ٱلرِّيَاحَ مُبَشِّرَٰتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحْمَتِهِۦ وَلِتَجْرِىَ ٱلْفُلْكُ بِأَمْرِهِۦ وَلِتَبْتَغُوا۟ مِن فَضْلِهِۦ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili kuwaonjesha baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yaende kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa katika Ishara zake ni kuzituma pepo ziletazo bishara njema, na ili kukuonjesheni baadhi ya rehema zake, na ili majahazi yende kwa amri yake; na mtafute kutokana na fadhila yake, na ili mumshukuru.