Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika tuliwajaribu waliokuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha wale walio wakweli na atawatambulisha waongo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kutaraji kukutana na Mwenyezi Mungu, basi hakika miadi ya Mwenyezi Mungu itafika bila ya shaka. Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa anayefanya juhudi, basi bila ya shaka anafanya juhudi kwa ajili ya nafsi yake. Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioamini na wakatenda mema, kwa yakini tutawafutia makosa yao, na bila shaka tutawalipa bora ya waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumemuusia mwanadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watapambana nawe ili unishirikishe Mimi na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Kwangu Mimi ndiyo marejeo yenu, na nitawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika watu yupo yule anayesema, "Tumemuamini Mwenyezi Mungu." Lakini anapopewa maudhi kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, anayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapokuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi, kwa yakini husema, "Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi." Kwani Mwenyezi Mungu hayajui zaidi yaliyomo vifuani mwa walimwengu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hapana shaka wataibeba mizigo yao na mizigo mingine pamoja na mizigo yao. Na kwa yakini wataulizwa Siku ya Kiyama juu ya yale waliyokuwa wakiyazua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, na akakaa nao miaka elfu kasoro miaka hamsini. Basi tufani ikawachukua, nao ni madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Ibrahim pale alipowaambia watu wake, "Muabuduni Mwenyezi Mungu, na mcheni Yeye. Hiyo ndiyo heri yenu, ikiwa nyinyi mnajua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika nyinyi mnaabudu tu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, na mnazua uzushi. Hakika hao mnaowaabudu badala ya Mwenyezi Mungu hawawamilikii riziki yoyote. Basi tafuteni riziki kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na mumshukuru Yeye. Kwake Yeye ndiko mtarudishwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mkikadhibisha, basi kaumu kadhaa wa kadhaa za kabla yenu zilikwisha kadhibisha. Na si juu ya Mtume isipokuwa kufikisha Ujumbe waziwazi."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, wao hawaoni jinsi Mwenyezi Mungu anavyoanzisha uumbaji, na kisha akaurudisha tena. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Tembeeni katika ardhi na tazameni jinsi alivyoanzisha uumbaji; kisha Mwenyezi Mungu ndiye anayeumba umbo la baadaye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliozikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu na kukutana naye, hao ndio waliokata tamaa na rehema yangu, na hao ndio wana adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi haikuwa jawabu ya watu wake isipokuwa walisema, "Muueni au mchomeni moto!" Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu akamwokoa kutokana na moto huo. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa watu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alisema, "Hakika nyinyi mmeyashika masanamu (kuyaabudu) badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yaliyo baina yenu katika uhai wa duniani. Kisha Siku ya Kiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi, na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi. Na makazi yenu ni Motoni. Wala hamtapata wa kukunusuru wowote."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLuti akamuamini, na akasema, "Hakika mimi nahamia kwa Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hekima."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulimtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaa'qub. Na tukajaalia katika dhuria zake Unabii na Kitabu, na tukampa ujira wake katika dunia; naye hakika katika Akhera bila ya shaka ni katika watu wema.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pale Luti alipowaambia watu wake, "Hakika nyinyi mnafanya uchafu, ambao hapana mmoja katika walimwengu aliyewatangulia kwa hayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, nyinyi mnawaingilia wanaume, na mnaikata njia? Na katika mikutano yenu mnafanya maovu?" Basi haikuwa jawabu ya watu wake isipokuwa walisema, "Tuletee hiyo adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwa wewe ni katika wakweli."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wajumbe wetu walipomjia Ibrahim na bishara, walisema, "Hakika sisi hapana shaka tutawaangamiza watu wa mji huu, kwani watu wake hakika wamekuwa madhalimu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAkasema, "Hakika humo yumo Luti." Wao wakasema, "Sisi tunajua zaidi ni nani yumo humo. Hapana shaka tutamwokoa yeye na ahali zake, isipokuwa mkewe aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wajumbe wetu walipomfikia Luti, alihuzunika kwa sababu yao, na moyo ukaona dhiki kubwa kwa sababu yao. Wakasema, "Usihofu, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, isipokuwa mkeo aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa yakini sisi tutawateremshia watu wa mji huu adhabu kutoka mbinguni kwa sababu ya kuvuka kwao mipaka."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa Madyana tulimtuma ndugu yao Shuaibu, naye akasema, "Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu na iogopeni Siku ya Akhera, wala msiende katika ardhi mkifanya uharibifu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini walimkadhibisha, basi ukawatwaa mtikiso wa ardhi, wakapambazukiwa ndani ya nyumba zao nao wameanguka kifudifudi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pia kina A'di na Thamud. Nanyi yamekwisha wabainikia kutokana na maskani zao. Na Shetani aliwapambia vitendo vyao, na akawazuilia Njia, na hali walikuwa wenye kuona.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pia Qaruni na Firauni na Hamana! Na Musa aliwajia kwa Ishara waziwazi, lakini walijivuna katika nchi, wala hawakuweza kushinda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kila mmoja tulimtesa kwa mujibu wa makosa yake. Kati yao wapo tuliowapelekea kimbunga cha changarawe; na kati yao wapo walionyakuliwa na ukelele; na kati yao wapo ambao tuliwadidimiza katika ardhi; na kati yao wapo tuliowazamisha. Wala Mwenyezi Mungu hakuwa mwenye kuwadhulumu, lakini walikuwa wenyewe wakijidhulumu nafsi zao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMfano wa wale waliowafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyojitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu wanachokiomba badala yake Yeye. Na Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSoma yale uliyofunuliwa katika Kitabu, na ushike Swala. Hakika Swala inazuilia mambo machafu na maovu. Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa. Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msijadiliane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni, "Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivyo tumekuteremshia Kitabu hiki (Qur-ani). Basi wale tuliowapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur-ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakaoiamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa makafiri.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wewe hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kulia. Ingelikuwa hivyo, wana batili wangelifanya shaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali hii (Qur-ani) ni Ishara zilizo wazi katika vifua vya wale waliopewa elimu. Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa madhalimu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walisema, "Mbona hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi?" Sema, "Hakika Ishara ziko tu kwake Mwenyezi Mungu; ama mimi kwa hakika ni mwonyaji mwenye kubainisha tu."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, kwani hayakuwatosha ya kwamba tumekuteremshia Kitabu hiki wanachosomewa? Hakika katika hayo, zipo rehema na mawaidha kwa watu wanaoamini.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema, "Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Shahidi kati yangu na nyinyi. Anayajua yaliyo katika mbingu na ardhi. Na wale wanaoiamini batili na wakamkufuru Mwenyezi Mungu, hao ndio waliohasiri."
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanakuhimiza waletewe adhabu kwa haraka. Na lau kuwa hapana wakati maalumu uliowekwa, basi adhabu ingeliwajia, na ingeliwatokea kwa ghafla ilhali wao hawana habari.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku itakapowafunika adhabu hiyo kutoka juu yao na chini ya miguu yao, na atasema, "Onjeni hayo mliyokuwa mkiyatenda!"
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao wameamini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Bustani ya mbinguni yenye kupitiwa chini yake mito, wakidumu humo. Ni mzuri ulioje huo ujira wa watendao.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni wanyama wangapi hawawezi kujimilikia riziki zao! Mwenyezi Mungu anawaruzuku hao na nyinyi pia. Na Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukiwauliza; ni nani aliyeumba mbingu na ardhi na akafanya jua na mwezi kutiii amri yake? Bila ya shaka, watasema: Mwenyezi Mungu. Wapi basi wanakogeuzwa?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu humkunjulia, na humkunjia riziki amtakaye katika waja wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ukiwauliza: Ni nani anayeteremsha maji kutoka mbinguni, na akaihuisha ardhi baada ya kufa kwake? Bila ya shaka watasema: Ni Mwenyezi Mungu. Sema: Alhamdu Lillahi (Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu). Bali wengi katika wao hawatumii akili.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa haya maisha ya dunia si chochote isipokuwa ni pumbao na mchezo. Na hakika nyumba ya Akhera ndiyo maisha hasa; laiti wangelikuwa wanajua!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanapopanda katika marikebu, humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumkusudia yeye tu dini yake. Lakini anapowavua wakafika nchi kavu, mara wanamshirikisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawaoni ya kwamba tumeifanya nchi takatifu ina amani, na hali watu wengine wananyakuliwa kote kwa majirani zao? Je, wanaamini batili, na neema za Mwenyezi Mungu wanazikufuru?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu au anayekadhibisha Haki inapomjia? Je, si katika Jahannamu ndiyo yatakuwa makazi ya makafiri?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi hakika tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.