فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا فِطْرَتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِى فَطَرَ ٱلنَّاسَ عَلَيْهَا لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ ٱللَّهِ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi uelekeze uso wako sawasawa kwenye Dini kwa unyoofu, ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu. Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo Dini iliyonyooka sawa. Lakini watu wengi hawajui.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi uwelekeze uso wako sawa sawa kwenye Dini. Ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilo waumbia watu, hapana mabadilko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndio Dini ilionyoka sawa, lakini watu wengi hawajui.