caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ar-Room, Aya 28

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 84 · 30:28

ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَٰنُكُم مِّن شُرَكَآءَ فِى مَا رَزَقْنَٰكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَآءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَٰتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmewapigia mfano kutokana na nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyowaruzuku, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivyo tunazipambanua Aya zetu kwa watu watumiao akili.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAmekupigieni mfano kutokana na nafsi zenu. Je! Katika hao iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia mnao washirika katika hivyo tulivyo kuruzukuni, mkawa nyinyi katika hivyo ni sawasawa, mnawaogopa kama mnavyo ogopana wenyewe kwa wenyewe? Namna hivi tunazipambanua Aya zetu kwa watu wenye akili.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70