caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Anfaal, Aya 48

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 88 · 8:48

وَإِذْ زَيَّنَ لَهُمُ ٱلشَّيْطَٰنُ أَعْمَٰلَهُمْ وَقَالَ لَا غَالِبَ لَكُمُ ٱلْيَوْمَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَإِنِّى جَارٌ لَّكُمْ فَلَمَّا تَرَآءَتِ ٱلْفِئَتَانِ نَكَصَ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ وَقَالَ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّنكُمْ إِنِّىٓ أَرَىٰ مَا لَا تَرَوْنَ إِنِّىٓ أَخَافُ ٱللَّهَ وَٱللَّهُ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakati Shetani alipowapambia vitendo vyao, na akasema, "Hakuna yeyote wa kuwashinda leo hii katika watu, nami hakika ni rafiki mlinzi wenu." Basi yalipoonana makundi mawili hayo, akarudi nyuma juu ya visigino vyake, na akasema, "Hakika mimi niko mbali sana nanyi. Hakika mimi naona msiyoyaona. Hakika mimi ninamhofu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa pale Shet'ani alipo wapambia vitendo vyao, na akawaambia: Hapana watu wa kukushindeni hii leo, na hali mimi ni mlinzi wenu. Yalipo onana majeshi mawili, akarudi nyuma, na akasema: Mimi si pamoja nanyi. Mimi naona msiyo yaona. Mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70