يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِىُّ حَرِّضِ ٱلْمُؤْمِنِينَ عَلَى ٱلْقِتَالِ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَٰبِرُونَ يَغْلِبُوا۟ مِا۟ئَتَيْنِ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّا۟ئَةٌ يَغْلِبُوٓا۟ أَلْفًا مِّنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterEwe Nabii! Wahimize Waumini juu ya kupigana vita. Wakiwapo miongoni mwenu ishirini wanaosubiri, watawashinda mia mbili. Na wakiwapo miongoni mwenu mia, watawashinda elfu moja katika wale waliokufuru, kwa sababu wao ni kaumu wasiofahamu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniEwe Nabii! Wahimize Waumini wende vitani. Wakiwapo kati yenu ishirini wanao subiri watawashinda mia mbili. Na wakiwapo kati yenu mia watawashinda elfu moja katika walio kufuru. Kwa sababu wao ni watu wasio fahamu.