كَدَأْبِ ءَالِ فِرْعَوْنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمْ فَأَهْلَكْنَٰهُم بِذُنُوبِهِمْ وَأَغْرَقْنَآ ءَالَ فِرْعَوْنَ وَكُلٌّ كَانُوا۟ ظَٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi kama ada ya watu wa Firauni na wale waliokuwa kabla yao, walizikadhibisha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawaangamiza kwa madhambi yao, na tukawazamisha watu wa Firauni. Na kila mmoja wao walikuwa madhalimu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNi kama ada ya watu wa Firauni na walio kabla yao - walizikanusha Ishara za Mola wao Mlezi, basi tukawateketeza kwa madhambi yao. Na tukawazamisha watu wa Firauni. Na wote walikuwa wenye kudhulumu.