caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Anfaal, Aya 42

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 88 · 8:42

إِذْ أَنتُم بِٱلْعُدْوَةِ ٱلدُّنْيَا وَهُم بِٱلْعُدْوَةِ ٱلْقُصْوَىٰ وَٱلرَّكْبُ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَلَوْ تَوَاعَدتُّمْ لَٱخْتَلَفْتُمْ فِى ٱلْمِيعَٰدِ وَلَٰكِن لِّيَقْضِىَ ٱللَّهُ أَمْرًا كَانَ مَفْعُولًا لِّيَهْلِكَ مَنْ هَلَكَ عَنۢ بَيِّنَةٍ وَيَحْيَىٰ مَنْ حَىَّ عَنۢ بَيِّنَةٍ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa kwenye ng'ambo ya mbali, na msafara ulipokuwa chini yenu. Na ingelikuwa mliagana, basi mngelihitilafiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe. Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio wazi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKumbukeni pale mlipo kuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa ng'ambo ya mbali, na msafara ulipo kuwa chini yenu. Na ingeli kuwa mmeagana mngeli khitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lilio kuwa lazima litendeke, kwa sababu aangamie wa kuangamia kwa dalili zilizo dhaahiri, na asalimike wa kusalimika kwa dalili zilizo dhaahiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70