caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Anfaal, Aya 60

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 88 · 8:60

وَأَعِدُّوا۟ لَهُم مَّا ٱسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ ٱلْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِۦ عَدُوَّ ٱللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَءَاخَرِينَ مِن دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ ٱللَّهُ يَعْلَمُهُمْ وَمَا تُنفِقُوا۟ مِن شَىْءٍ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لَا تُظْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waandalieni muwezavyo katika nguvu, na kwa farasi waliofungwa tayari tayari, ili muwatie hofu kwavyo maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo kando na hao ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na chochote mnachotoa kwenda katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mtarudishiwa kikamilifu, nanyi hamtadhulumiwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniBasi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70