إِن تَسْتَفْتِحُوا۟ فَقَدْ جَآءَكُمُ ٱلْفَتْحُ وَإِن تَنتَهُوا۟ فَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ وَإِن تَعُودُوا۟ نَعُدْ وَلَن تُغْنِىَ عَنكُمْ فِئَتُكُمْ شَيْـًٔا وَلَوْ كَثُرَتْ وَأَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMkiomba msaada wa ushindi, basi msaada wa ushindi ulikwishawajia. Na mkikomeka, basi hilo ndilo heri kwenu. Na mkirejea, Sisi pia tutarejea. Na kundi lenu halitawanufaisha kitu hata kama yatakuwa (makundi) mengi. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniKama mnataka hukumu basi hukumu imekwisha kujieni. Na mkiacha itakuwa ndio kheri kwenu. Na mkirejea Sisi pia tutarejea. Na jeshi lenu halitakufaeni kitu, japo likiwa kubwa. Kwani hakika Mwenyezi yu pamoja na Waumini.