caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Ghaafir غافر

Aya 85 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 60

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ حمٓ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHa Mim.[1]

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَنزِيلُ ٱلْكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْعَلِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterUteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua vyema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

غَافِرِ ٱلذَّنۢبِ وَقَابِلِ ٱلتَّوْبِ شَدِيدِ ٱلْعِقَابِ ذِى ٱلطَّوْلِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ إِلَيْهِ ٱلْمَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayesamehe dhambi na anayepokea toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye ukarimu, hakuna mungu ila Yeye; marejeo ni kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَا يُجَٰدِلُ فِىٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِى ٱلْبِلَٰدِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawazibishi Ishara za Mwenyezi Mungu ila wale waliokufuru; basi kusikudanganye wewe kutangatanga kwao katika nchi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَٱلْأَحْزَابُ مِنۢ بَعْدِهِمْ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍۭ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ وَجَٰدَلُوا۟ بِٱلْبَٰطِلِ لِيُدْحِضُوا۟ بِهِ ٱلْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuhu na makundi mengine baada yao. Na kila taifa lilikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate. Na walibishana kwa upotovu ili kuipindua haki. Kwa hivyo niliwakamata. Basi ilikuwaje adhabu yangu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ أَنَّهُمْ أَصْحَٰبُ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNamna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako Mlezi ya kwamba wao ni watu wa Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يَحْمِلُونَ ٱلْعَرْشَ وَمَنْ حَوْلَهُۥ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيُؤْمِنُونَ بِهِۦ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَىْءٍ رَّحْمَةً وَعِلْمًا فَٱغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا۟ وَٱتَّبَعُوا۟ سَبِيلَكَ وَقِهِمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale wanaobeba Kiti cha Enzi, na wale walio pembezoni mwake, wanamsabihi na kumhimidi Mola wao Mlezi, na wanamuamini, na wanawaombea msamaha walioamini kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe wale waliotubu na wakaifuata Njia yako, na waepushe na adhabu ya Jahanamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّٰتِ عَدْنٍ ٱلَّتِى وَعَدتَّهُمْ وَمَن صَلَحَ مِنْ ءَابَآئِهِمْ وَأَزْوَٰجِهِمْ وَذُرِّيَّٰتِهِمْ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْعَزِيزُ ٱلْحَكِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMola wetu Mlezi! Na waingize katika Bustani za Milele ulizowaahidi. Na uwape haya pia wale waliofanya mema miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقِهِمُ ٱلسَّيِّـَٔاتِ وَمَن تَقِ ٱلسَّيِّـَٔاتِ يَوْمَئِذٍ فَقَدْ رَحِمْتَهُۥ وَذَٰلِكَ هُوَ ٱلْفَوْزُ ٱلْعَظِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waepushe na maovu; kwani umwepushaye maovu siku hiyo, hakika umemrehemu; na huko ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُنَادَوْنَ لَمَقْتُ ٱللَّهِ أَكْبَرُ مِن مَّقْتِكُمْ أَنفُسَكُمْ إِذْ تُدْعَوْنَ إِلَى ٱلْإِيمَٰنِ فَتَكْفُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika wale waliokufuru watanadiwa: Bila ya shaka kukuchukieni Mwenyezi Mungu ni kukubwa kuliko kujichukia nyinyi nafsi zenu, mlipokuwa mnaitwa kwenye Imani nanyi mnakufuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوا۟ رَبَّنَآ أَمَتَّنَا ٱثْنَتَيْنِ وَأَحْيَيْتَنَا ٱثْنَتَيْنِ فَٱعْتَرَفْنَا بِذُنُوبِنَا فَهَلْ إِلَىٰ خُرُوجٍ مِّن سَبِيلٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema: Mola wetu Mlezi! Umetufisha mara mbili, na umetuhuisha mara mbili! Basi tunakiri madhambi yetu. Basi je, ipo njia yoyote ya kutoka?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكُم بِأَنَّهُۥٓ إِذَا دُعِىَ ٱللَّهُ وَحْدَهُۥ كَفَرْتُمْ وَإِن يُشْرَكْ بِهِۦ تُؤْمِنُوا۟ فَٱلْحُكْمُ لِلَّهِ ٱلْعَلِىِّ ٱلْكَبِيرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni hivyo kwa sababu mlikuwa akiombwa Mwenyezi Mungu peke yake mnakataa. Na akishirikishwa mnaamini. Basi hukumu ni ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Mkuu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِى يُرِيكُمْ ءَايَٰتِهِۦ وَيُنَزِّلُ لَكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ رِزْقًا وَمَا يَتَذَكَّرُ إِلَّا مَن يُنِيبُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye anayekuonyesheni Ishara zake, na anakuteremshieni kutoka mbinguni riziki. Na hapana anayekumbuka ila anayerejea kwa toba.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱدْعُوا۟ ٱللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ وَلَوْ كَرِهَ ٱلْكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mwombeni Mwenyezi Mungu mkimsafia Dini Yeye tu, na wangalichukia makafiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

رَفِيعُ ٱلدَّرَجَٰتِ ذُو ٱلْعَرْشِ يُلْقِى ٱلرُّوحَ مِنْ أَمْرِهِۦ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنْ عِبَادِهِۦ لِيُنذِرَ يَوْمَ ٱلتَّلَاقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye Mwenye vyeo vya juu, Mwenye 'Arshi. Hutuma Roho kwa amri yake juu ya amtakaye katika waja wake, ili kuonya kwa Siku ya Mkutano.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ هُم بَٰرِزُونَ لَا يَخْفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِنْهُمْ شَىْءٌ لِّمَنِ ٱلْمُلْكُ ٱلْيَوْمَ لِلَّهِ ٱلْوَٰحِدِ ٱلْقَهَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku watakayodhihiri wao. Hapana kitakachofichikana chochote chao kwa Mwenyezi Mungu. Ufalme ni wa nani leo? Ni wa Mwenyezi Mungu, Mmoja, Mshindi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلْيَوْمَ تُجْزَىٰ كُلُّ نَفْسٍۭ بِمَا كَسَبَتْ لَا ظُلْمَ ٱلْيَوْمَ إِنَّ ٱللَّهَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLeo kila nafsi italipwa kwa yale iliyochuma. Hapana dhuluma leo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kufanya hesabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَنذِرْهُمْ يَوْمَ ٱلْـَٔازِفَةِ إِذِ ٱلْقُلُوبُ لَدَى ٱلْحَنَاجِرِ كَٰظِمِينَ مَا لِلظَّٰلِمِينَ مِنْ حَمِيمٍ وَلَا شَفِيعٍ يُطَاعُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa waonye siku inayokurubia, wakati nyoyo zitakapofika kooni, nao wamejaa huzuni. Madhalimu hawatakuwa na rafiki, wala mwombezi wa kuitikiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَعْلَمُ خَآئِنَةَ ٱلْأَعْيُنِ وَمَا تُخْفِى ٱلصُّدُورُ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Mwenyezi Mungu) anajua hiyana ya macho na yale ambayo vifua vinayaficha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ يَقْضِى بِٱلْحَقِّ وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَقْضُونَ بِشَىْءٍ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْبَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu huhukumu kwa haki; lakini hao ambao wao wanawaomba badala yake hawahukumu chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ كَانُوا۟ مِن قَبْلِهِمْ كَانُوا۟ هُمْ أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَءَاثَارًا فِى ٱلْأَرْضِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمْ وَمَا كَانَ لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawatembei katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Hao walikuwa wamewazidi hawa kwa nguvu na athari katika nchi. Na Mwenyezi Mungu aliwatia mkononi kwa sababu ya madhambi yao. Na wala hapakuwa wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ فَكَفَرُوا۟ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ إِنَّهُۥ قَوِىٌّ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ni kwa sababu walikuwa Mitume wao walikuwa wanawajia kwa hoja zilizo wazi, lakini wakawakataa, ndipo Mwenyezi Mungu akawakamata. Bila ya shaka Yeye ni Mwenye nguvu, Mkali wa kuadhibu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَا وَسُلْطَٰنٍ مُّبِينٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa yakini tulimtuma Musa pamoja na Ishara zetu na uthibitisho ulio wazi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَهَٰمَٰنَ وَقَٰرُونَ فَقَالُوا۟ سَٰحِرٌ كَذَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKumwendea Firauni na Hamana na Qaruni, wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلْحَقِّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا۟ ٱقْتُلُوٓا۟ أَبْنَآءَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مَعَهُۥ وَٱسْتَحْيُوا۟ نِسَآءَهُمْ وَمَا كَيْدُ ٱلْكَٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَٰلٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi alipowaletea Haki inayotoka kwetu, walisema: "Waueni watoto wanaume wa wale waliomuamini na wawacheni hai wanawake wao." Na haviwi vitimbi vya makafiri ila katika upotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ فِرْعَوْنُ ذَرُونِىٓ أَقْتُلْ مُوسَىٰ وَلْيَدْعُ رَبَّهُۥٓ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُبَدِّلَ دِينَكُمْ أَوْ أَن يُظْهِرَ فِى ٱلْأَرْضِ ٱلْفَسَادَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Firauni akasema: Niachieni nimuue Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi nachelea asije kubadilishieni dini yenu, au akadhihirisha uharibifu katika nchi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ مُوسَىٰٓ إِنِّى عُذْتُ بِرَبِّى وَرَبِّكُم مِّن كُلِّ مُتَكَبِّرٍ لَّا يُؤْمِنُ بِيَوْمِ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Musa akasema: Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi anilinde na kila mwenye jeuri asiyeiamini Siku ya Hesabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ رَجُلٌ مُّؤْمِنٌ مِّنْ ءَالِ فِرْعَوْنَ يَكْتُمُ إِيمَٰنَهُۥٓ أَتَقْتُلُونَ رَجُلًا أَن يَقُولَ رَبِّىَ ٱللَّهُ وَقَدْ جَآءَكُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ مِن رَّبِّكُمْ وَإِن يَكُ كَٰذِبًا فَعَلَيْهِ كَذِبُهُۥ وَإِن يَكُ صَادِقًا يُصِبْكُم بَعْضُ ٱلَّذِى يَعِدُكُمْ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ كَذَّابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akasema mwanamume mmoja Muumini, aliyekuwa mmoja katika watu wa Firauni aliyeficha Imani yake: Mtamuuwa mtu kwa sababu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu? Na hali naye amekujieni na hoja zilizo wazi? Na akiwa yeye mwongo, basi uongo wake ni juu yake mwenyewe. Na akiwa mkweli, yatakufikieni baadhi ya hayo anayokuahidini. Hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi apitilizaye mipaka, mwongo mkubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰقَوْمِ لَكُمُ ٱلْمُلْكُ ٱلْيَوْمَ ظَٰهِرِينَ فِى ٱلْأَرْضِ فَمَن يَنصُرُنَا مِنۢ بَأْسِ ٱللَّهِ إِن جَآءَنَا قَالَ فِرْعَوْنُ مَآ أُرِيكُمْ إِلَّا مَآ أَرَىٰ وَمَآ أَهْدِيكُمْ إِلَّا سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu wangu! Leo mna ufalme, mmeshinda katika nchi; basi ni nani atakayenisaidia kutuokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kama ikitufikia? Firauni akasema: Sikupeni shauri ila ile niliyoiona, wala siwaongozi ila kwenye njia ya uongofu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِىٓ ءَامَنَ يَٰقَوْمِ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُم مِّثْلَ يَوْمِ ٱلْأَحْزَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akasema yule aliyeamini: Enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia mfano wa siku za makundi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِثْلَ دَأْبِ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ وَٱلَّذِينَ مِنۢ بَعْدِهِمْ وَمَا ٱللَّهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعِبَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMfano wa hali ya watu wa Nuhu na 'Adi na Thamudi na wale wa baada yao. Na Mwenyezi Mungu hataki kuwadhulumu waja.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَٰقَوْمِ إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ يَوْمَ ٱلتَّنَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa enyi watu wangu! Hakika mimi nawahofia Siku ya mayowe.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ تُوَلُّونَ مُدْبِرِينَ مَا لَكُم مِّنَ ٱللَّهِ مِنْ عَاصِمٍ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنْ هَادٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku mtakapogeuka kurudi nyuma. Hamtakuwa na wa kukulindeni kutokana na Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuhukumiwa na Mwenyezi Mungu kupotea, basi huyo hana wa kumwongoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ جَآءَكُمْ يُوسُفُ مِن قَبْلُ بِٱلْبَيِّنَٰتِ فَمَا زِلْتُمْ فِى شَكٍّ مِّمَّا جَآءَكُم بِهِۦ حَتَّىٰٓ إِذَا هَلَكَ قُلْتُمْ لَن يَبْعَثَ ٱللَّهُ مِنۢ بَعْدِهِۦ رَسُولًا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَنْ هُوَ مُسْرِفٌ مُّرْتَابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa alikwisha wajieni Yusuf zamani kwa dalili zilizo wazi, lakini nyinyi mliendelea katika shaka kwa yale aliyokuleteeni; mpaka alipokufa, mkasema: Mwenyezi Mungu hataleta kabisa Mtume baada yake. Kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha kupotea anayepindukia mipaka katika maasi anayejitia shaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِىٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَٰنٍ أَتَىٰهُمْ كَبُرَ مَقْتًا عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHao ambao wanajadiliana katika Ishara za Mwenyezi Mungu pasipo ushahidi wowote uliowafikia, ni chukizo kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya wale walioamini. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu azibavyo kila moyo wa jeuri anayejivuna.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَٰهَٰمَٰنُ ٱبْنِ لِى صَرْحًا لَّعَلِّىٓ أَبْلُغُ ٱلْأَسْبَٰبَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Firauni akasema: Ewe Hamana! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَسْبَٰبَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰٓ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّى لَأَظُنُّهُۥ كَٰذِبًا وَكَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِفِرْعَوْنَ سُوٓءُ عَمَلِهِۦ وَصُدَّ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَا كَيْدُ فِرْعَوْنَ إِلَّا فِى تَبَابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNjia za mbinguni ili nikamwone Mungu wa Musa. Na kwa hakika mimi bila ya shaka namjua kuwa ni mwongo tu. Na hivi ndivyo Firauni alivyopambiwa ubaya wa vitendo vyake, na akazuiliwa Njia. Na vitimbi vya Firauni havikuwa ila katika kuangamia tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِىٓ ءَامَنَ يَٰقَوْمِ ٱتَّبِعُونِ أَهْدِكُمْ سَبِيلَ ٱلرَّشَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yule aliyeamini alisema: Enyi watu wangu! Nifuateni mimi, nitakuongozeni njia ya uongozi mwema.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَٰقَوْمِ إِنَّمَا هَٰذِهِ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا مَتَٰعٌ وَإِنَّ ٱلْـَٔاخِرَةَ هِىَ دَارُ ٱلْقَرَارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterEnyi watu wangu! Hakika haya maisha ya dunia ni starehe ipitayo tu, na hakika Akhera ndiyo nyumba ya daima.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰٓ إِلَّا مِثْلَهَا وَمَنْ عَمِلَ صَٰلِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُو۟لَٰٓئِكَ يَدْخُلُونَ ٱلْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye kutenda uovu, hatalipwa ila sawa na huo uovu wake. Na anayetenda wema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Peponi, waruzukiwe humo bila ya hesabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَٰقَوْمِ مَا لِىٓ أَدْعُوكُمْ إِلَى ٱلنَّجَوٰةِ وَتَدْعُونَنِىٓ إِلَى ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa enyi watu wangu! Kwa nini mimi nakuiteni kwenye wokovu, nanyi mnaniita kwenye Moto?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَدْعُونَنِى لِأَكْفُرَ بِٱللَّهِ وَأُشْرِكَ بِهِۦ مَا لَيْسَ لِى بِهِۦ عِلْمٌ وَأَنَا۠ أَدْعُوكُمْ إِلَى ٱلْعَزِيزِ ٱلْغَفَّٰرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMnaniita nimkufuru Mwenyezi Mungu na nimshirikishe na yule ambaye simjui, nami nakuiteni kwa Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe mno?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَا جَرَمَ أَنَّمَا تَدْعُونَنِىٓ إِلَيْهِ لَيْسَ لَهُۥ دَعْوَةٌ فِى ٱلدُّنْيَا وَلَا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَنَّ مَرَدَّنَآ إِلَى ٱللَّهِ وَأَنَّ ٱلْمُسْرِفِينَ هُمْ أَصْحَٰبُ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka mnayeniitia kumuabudu hastahiki wito duniani wala Akhera. Na hakika marejeo yetu ni kwa Mwenyezi Mungu. Na wanaopindukia mipaka ndio watu wa Motoni!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَسَتَذْكُرُونَ مَآ أَقُولُ لَكُمْ وَأُفَوِّضُ أَمْرِىٓ إِلَى ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ بَصِيرٌۢ بِٱلْعِبَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi mtayakumbuka ninayokuambieni. Nami namkabidhi Mwenyezi Mungu mambo yangu. Hakika Mwenyezi Mungu anawaona vyema waja wake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَوَقَىٰهُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِ مَا مَكَرُوا۟ وَحَاقَ بِـَٔالِ فِرْعَوْنَ سُوٓءُ ٱلْعَذَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Mwenyezi Mungu akamlinda kutokana na ubaya wa hila walizozifanya. Na adhabu mbaya itawazingira watu wa Firauni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلنَّارُ يُعْرَضُونَ عَلَيْهَا غُدُوًّا وَعَشِيًّا وَيَوْمَ تَقُومُ ٱلسَّاعَةُ أَدْخِلُوٓا۟ ءَالَ فِرْعَوْنَ أَشَدَّ ٱلْعَذَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWanaonyeshwa Moto asubuhi na jioni. Na itapofika Saa ya Kiyama, patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِذْ يَتَحَآجُّونَ فِى ٱلنَّارِ فَيَقُولُ ٱلضُّعَفَٰٓؤُا۟ لِلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا لَكُمْ تَبَعًا فَهَلْ أَنتُم مُّغْنُونَ عَنَّا نَصِيبًا مِّنَ ٱلنَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa watakapohojiana huko Motoni, wanyonge watawaambia wale waliojitukuza: Hakika sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, hamtuondolei sehemu ya huu Moto?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسْتَكْبَرُوٓا۟ إِنَّا كُلٌّ فِيهَآ إِنَّ ٱللَّهَ قَدْ حَكَمَ بَيْنَ ٱلْعِبَادِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWatasema wale waliojitukuza: Hakika sote sisi tumo humo humo! Kwani Mwenyezi Mungu ameshahukumu baina ya waja!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ ٱلَّذِينَ فِى ٱلنَّارِ لِخَزَنَةِ جَهَنَّمَ ٱدْعُوا۟ رَبَّكُمْ يُخَفِّفْ عَنَّا يَوْمًا مِّنَ ٱلْعَذَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walio Motoni watawaambia walinzi wa Jahannamu: Mwombeni Mola wenu Mlezi atupunguzie walau siku moja ya adhabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قَالُوٓا۟ أَوَلَمْ تَكُ تَأْتِيكُمْ رُسُلُكُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ قَالُوا۟ بَلَىٰ قَالُوا۟ فَٱدْعُوا۟ وَمَا دُعَٰٓؤُا۟ ٱلْكَٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَٰلٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao watasema: Je, hawakuwa wakikufikieni Mitume wenu kwa hoja zilizo wazi? Watasema: Kwani? Watasema: Basi ombeni! Na maombi ya makafiri hayawi ila ni kupotea bure.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّا لَنَنصُرُ رُسُلَنَا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَيَوْمَ يَقُومُ ٱلْأَشْهَٰدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika bila ya shaka Sisi tunawanusuru Mitume wetu na wale walioamini katika uhai wa duniani na siku watakaposimama Mashahidi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَوْمَ لَا يَنفَعُ ٱلظَّٰلِمِينَ مَعْذِرَتُهُمْ وَلَهُمُ ٱللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوٓءُ ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao, nao watapata laana, na watapata makazi mabaya kabisa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْهُدَىٰ وَأَوْرَثْنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱلْكِتَٰبَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa hakika tulimpa Musa uongofu, na tukawarithisha Wana wa Israili Kitabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُدًى وَذِكْرَىٰ لِأُو۟لِى ٱلْأَلْبَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbacho ni Uongofu na Ukumbusho kwa wenye akili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ وَٱسْتَغْفِرْ لِذَنۢبِكَ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ بِٱلْعَشِىِّ وَٱلْإِبْكَٰرِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli. Na omba msamaha kwa dhambi zako, na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi jioni na asubuhi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِىٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ بِغَيْرِ سُلْطَٰنٍ أَتَىٰهُمْ إِن فِى صُدُورِهِمْ إِلَّا كِبْرٌ مَّا هُم بِبَٰلِغِيهِ فَٱسْتَعِذْ بِٱللَّهِ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْبَصِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika hao wanaobishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya uthibitisho wowote uliowajia, hawana vifuani mwao ila kutaka ukubwa tu, na wala huo hawaufikilii. Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَخَلْقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBila ya shaka kuumba mbingu na ardhi ni kukubwa zaidi kuliko kuwaumba watu. Lakini watu wengi hawajui.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَلَا ٱلْمُسِىٓءُ قَلِيلًا مَّا تَتَذَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kipofu na mwenye kuona hawalingani; na wale walioamini na wakatenda mema hawalingani na muovu. Ni machache mnayoyakumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَـَٔاتِيَةٌ لَّا رَيْبَ فِيهَا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Saa (ya Kiyama) itafika, nayo haina shaka. Lakini watu wengi hawaamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَالَ رَبُّكُمُ ٱدْعُونِىٓ أَسْتَجِبْ لَكُمْ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِى سَيَدْخُلُونَ جَهَنَّمَ دَاخِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna wakaacha kuniabudu Mimi wataingia Jahanamu wadhalilike.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيْلَ لِتَسْكُنُوا۟ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبْصِرًا إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَشْكُرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye aliyewafanyia usiku ili mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ خَٰلِقُ كُلِّ شَىْءٍ لَّآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; basi mnageuzwa wapi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ يُؤْفَكُ ٱلَّذِينَ كَانُوا۟ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ يَجْحَدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNamna hivi ndivyo walivyogeuzwa wale waliokuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ قَرَارًا وَٱلسَّمَآءَ بِنَآءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَٰتِ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبُّكُمْ فَتَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi Mwenyezi Mungu aliyekufanyieni ardhi kuwa ni pahala pa kukaa, na mbingu kuwa dari. Na akawatia sura, na akazifanya nzuri sura zenu, na akawaruzuku vitu vizuri. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu Mlezi. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلْحَىُّ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱدْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ ٱلْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliye Hai - hapana mungu isipokuwa Yeye. Basi muabuduni Yeye mkimsafishia Dini Yeye. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ إِنِّى نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ ٱلَّذِينَ تَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَمَّا جَآءَنِىَ ٱلْبَيِّنَٰتُ مِن رَّبِّى وَأُمِرْتُ أَنْ أُسْلِمَ لِرَبِّ ٱلْعَٰلَمِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Mimi nimekatazwa kuwaabudu hao mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu, ziliponijia hoja zilizo dhahiri kutokana na Mola wangu Mlezi. Na nimeamrishwa nisilimu kwa Mola wa walimwengu wote.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِى خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ مِن نُّطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوٓا۟ أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا۟ شُيُوخًا وَمِنكُم مَّن يُتَوَفَّىٰ مِن قَبْلُ وَلِتَبْلُغُوٓا۟ أَجَلًا مُّسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye aliyewaumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha kwa pande la damu, kisha akawatoa katika hali ya mtoto mchanga, kisha mpate kufikilia utu uzima, kisha mpate kuwa wazee. Na kati yenu wapo wanaokufa kabla, na ili mfikie muda uliokwisha wekwa, na ili mpate kufahamu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِى يُحْىِۦ وَيُمِيتُ فَإِذَا قَضَىٰٓ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye anayehuisha na anayefisha. Akihukumu jambo liwe, basi huliambia: "Kuwa!" Likawa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُجَٰدِلُونَ فِىٓ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ أَنَّىٰ يُصْرَفُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, huwaoni wale wanaobishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu? Wanageuziwa wapi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِٱلْكِتَٰبِ وَبِمَآ أَرْسَلْنَا بِهِۦ رُسُلَنَا فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbao wamekanusha Kitabu na yale tuliyowatuma Mitume wetu. Basi watakuja jua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذِ ٱلْأَغْلَٰلُ فِىٓ أَعْنَٰقِهِمْ وَٱلسَّلَٰسِلُ يُسْحَبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterZitakapokuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى ٱلْحَمِيمِ ثُمَّ فِى ٱلنَّارِ يُسْجَرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ قِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تُشْرِكُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterTena wataambiwa: Wako wapi wale mliokuwa mkiwashirikisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مِن دُونِ ٱللَّهِ قَالُوا۟ ضَلُّوا۟ عَنَّا بَل لَّمْ نَكُن نَّدْعُوا۟ مِن قَبْلُ شَيْـًٔا كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلْكَٰفِرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBadala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea, bali tangu zamani hatukuwa tukiomba kitu! Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anawaachia makafiri wapotelee mbali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذَٰلِكُم بِمَا كُنتُمْ تَفْرَحُونَ فِى ٱلْأَرْضِ بِغَيْرِ ٱلْحَقِّ وَبِمَا كُنتُمْ تَمْرَحُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHaya ni kwa sababu mlikuwa mkijitapa katika ardhi pasipo haki, na kwa sababu mlikuwa mkijishaua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱدْخُلُوٓا۟ أَبْوَٰبَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَا فَبِئْسَ مَثْوَى ٱلْمُتَكَبِّرِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterIngieni kwenye milango ya Jahanamu, mdumu humo milele. Basi ni maovu yaliyoje makazi ya wanaotakabari!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَٱصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ ٱللَّهِ حَقٌّ فَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا يُرْجَعُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi subiri, hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli. Na ama tukikuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukikufisha, lakini wao watarudishwa kwetu tu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ مِنْهُم مَّن قَصَصْنَا عَلَيْكَ وَمِنْهُم مَّن لَّمْ نَقْصُصْ عَلَيْكَ وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِىَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ فَإِذَا جَآءَ أَمْرُ ٱللَّهِ قُضِىَ بِٱلْحَقِّ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلْمُبْطِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bila ya shaka tuliwatuma Mitume kabla yako. Wengine katika hao tumekusimulia habari zao, na wengine hatukukusimulia. Na haiwi Mtume alete Ishara yoyote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Basi ikija amri ya Mwenyezi Mungu, huhukumiwa kwa Haki, na hapo wapotovu watahasiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَنْعَٰمَ لِتَرْكَبُوا۟ مِنْهَا وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu aliyewajaalia nyama hoa, mifugo, ili muwapande baadhi yao, na muwale baadhi yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَكُمْ فِيهَا مَنَٰفِعُ وَلِتَبْلُغُوا۟ عَلَيْهَا حَاجَةً فِى صُدُورِكُمْ وَعَلَيْهَا وَعَلَى ٱلْفُلْكِ تُحْمَلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika hao mnayo manufaa kadhaa wa kadhaa, na mnapata kwao haja zilizomo vifuani mwenu; na mnachukuliwa juu yao, na juu ya merikebu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيُرِيكُمْ ءَايَٰتِهِۦ فَأَىَّ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ تُنكِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye anawaonyesha Ishara zake. Basi Ishara gani za Mwenyezi Mungu mnazozikataa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَيَنظُرُوا۟ كَيْفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ كَانُوٓا۟ أَكْثَرَ مِنْهُمْ وَأَشَدَّ قُوَّةً وَءَاثَارًا فِى ٱلْأَرْضِ فَمَآ أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwani hawatembei katika ardhi wakaona namna ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Wao walikuwa wengi kuliko hawa, na wamewashinda kwa nguvu na athari katika nchi. Wala hayakuwafaa hayo waliyokuwa wakiyachuma.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا جَآءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِٱلْبَيِّنَٰتِ فَرِحُوا۟ بِمَا عِندَهُم مِّنَ ٱلْعِلْمِ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipowajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, walijitapa kwa elimu waliyokuwa nayo. Basi yakawazingira yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمَّا رَأَوْا۟ بَأْسَنَا قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَحْدَهُۥ وَكَفَرْنَا بِمَا كُنَّا بِهِۦ مُشْرِكِينَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipoiona adhabu yetu, walisema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni wa pekee, na tunaikataa miungu tuliyokuwa tukiishirikisha naye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَلَمْ يَكُ يَنفَعُهُمْ إِيمَٰنُهُمْ لَمَّا رَأَوْا۟ بَأْسَنَا سُنَّتَ ٱللَّهِ ٱلَّتِى قَدْ خَلَتْ فِى عِبَادِهِۦ وَخَسِرَ هُنَالِكَ ٱلْكَٰفِرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini imani yao haikuwa yenye kuwafaa kitu wakati ambao wamekwisha iona adhabu yetu. Huu ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu uliokuwa kwa waja wake. Na hapo waliokufuru walihasiri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70