Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayotuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi hakika tunatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; inafunuliwa kwangu ya kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Basi nyookeni sawa kumwendea Yeye, na mumtake msamaha, na ole wao wanaomshirikisha.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Hivyo nyinyi mnamkataa yule aliyeumba ardhi katika siku mbili, na mnamfanyia washirika? Huyu ndiye Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaweka humo milima juu yake, na akabarikia humo na akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Haya ni sawa kabisa kwa wanaouliza.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo na ardhi: Njooni, kwa hiari au kwa nguvu! Vyote viwili vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi akazifanya mbingu saba kwa siku mbili, na akazipangia kila mbingu mambo yake. Na tukaipamba mbingu ya chini kwa mataa na kwa ulinzi. Hiki ndicho kipimo cha Mwenye Nguvu, ajuaye zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipowajia Mitume mbele yao na nyuma yao wakawaambia: Msimuabudu ila Mwenyezi Mungu! Wakasema: Angelitaka Mola wetu Mlezi, bila ya shaka angeliwateremsha Malaika. Basi sisi hakika tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAma kina 'Adi, hao walijivuna katika nchi bila ya haki, na wakasema: Ni nani mwenye nguvu kushinda sisi? Kwani wao hawakuona kwamba Mwenyezi Mungu aliyewaumba ni Mwenye nguvu kushinda wao? Na wao wakawa wanazikataa Ishara zetu!
Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi tukawatumia upepo wa kimbunga katika siku za misiba, ili tuwaonjeshe adhabu ya kuwahizi katika uhai wa duniani, na bila ya shaka adhabu ya Akhera ina hizaya zaidi, na wala wao hawatanusuriwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ama Thamudi, hao tuliwaongoza, lakini walipendelea upofu kuliko uongofu. Basi ukawachukua moto wa adhabu ya kuwafedhehesha kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHata watakapoufikia Moto, yatawashuhudia masikio yao, na macho yao na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao wataziambia ngozi zao: Kwa nini mmetushuhudilia? Nazo zitasema: Ametutamkisha Mwenyezi Mungu ambaye alitamkisha kila kitu! Na Yeye ndiye aliyewaumba mara ya kwanza, na kwake Yeye tu mtarejeshwa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hamkuwa wenye kujificha hata masikio yenu, na macho yenu, na ngozi zenu, zisikushuhudilieni. Lakini mlidhani kwamba Mwenyezi Mungu hayajui mengi katika yale mliyokuwa mkiyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukawawekea marafiki, na wakawapambia yaliyo mbele yao na nyuma yao. Basi ikawathibitikia kauli wawe pamoja na mataifa yaliyopita kabla yao, miongoni mwa majini na watu. Hakika hao wamekuwa ni wenye kuhasirika.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHayo ndiyo malipo ya Maadui wa Mwenyezi Mungu - Moto! Humo watakuwa na maskani ya kudumu, ndiyo malipo yao kwa sababu walikuwa wakizikataa Ishara zetu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru watasema: Mola wetu Mlezi! Tuonyeshe wale waliotupoteza miongoni mwa majini na watu ili tuwaweke chini ya miguu yetu, wapate kuwa miongoni wa walio chini kabisa.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinachotamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyovitaka.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ni nani mbora zaidi wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lililo jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Shetani akikuchochea kwa uchochezi, wewe jikinge kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, ajuaye zaidi.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Basi msilisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Mwenyezi Mungu aliyeviumba, ikiwa nyinyi mnamuabudu Yeye tu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa watajivuna, basi hao walioko kwa Mola wako Mlezi wanamtakasa Yeye usiku na mchana, na wao hawachoki.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika Ishara zake ni kwamba unaiona ardhi nyonge, lakini tunapoiteremshia maji, mara unaiona inataharaki na kuumuka. Bila ya shaka yule aliyeihuisha ardhi ndiye atakayehuisha wafu. Hakika Yeye ni Muweza mno wa kila kitu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika wale wanaopindukia mipaka katika Ishara zetu, hawafichikani kwetu. Je, atakayetupwa Motoni ni bora au atakayekuja kwa amani Siku ya Kiyama? Tendeni mpendavyo, kwa hakika Yeye anayaona vyema mnayoyatenda.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterKwa hakika wale walioyakufuru mawaidha haya yanapowajia (wataangamia), na haya bila ya shaka ni Kitabu chenye nguvu na utukufu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHuambiwi ila yale yale waliyoambiwa Mitume wa kabla yako. Hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ni Mwenye maghfira, na ni Mwenye adhabu chungu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa lau tungeliifanya Qur-ani kwa lugha ya kigeni, wangelisema: Kwa nini Aya zake hazikupambanuliwa? Yawaje lugha ya kigeni na Mtume Mwaarabu? Sema: Hii Qur-ani ni uongofu na ponya kwa wenye kuamini. Na wale wasioamini umo uziwi katika masikio yao, nayo kwao imezibwa hawaioni. Hao wanaitwa nao wako pahala mbali.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika tulimpa Musa Kitabu, lakini pakatokea tofauti juu yake. Na lau kuwa halikwisha tangulia neno la Mola wako Mlezi, wangelihukumiwa. Na hakika wao wamo katika shaka yenye kuwatia wasiwasi juu yake.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAnayetenda mema, basi anajitendea mwenyewe nafsi yake. Na mwenye kutenda uovu, basi ni juu ya nafsi yake vile vile; wala Mola wako Mlezi si mwenye kuwadhulumu waja.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterUjuzi wa kuijua Saa ya Kiyama unarudishwa kwake tu Mwenyezi Mungu. Na matunda hayatoki katika mafumba yake, wala cha kike hakichukui mimba, wala hakizai, ila kwa kujua kwake. Na siku atakayowaita, akawaambia: 'Wako wapi washirika wangu?' Hapo watasema: 'Tunakiri kwako ya kwamba hapana miongoni mwetu anayeshuhudia hayo.'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pindi tukimwonjesha rehema itokayo kwetu baada ya dhara kumgusa, bila ya shaka husema: 'Haya nayastahiki mimi, wala sidhani kuwa Kiyama kitakuja. Na hata nikirudishwa kwa Mola wangu Mlezi, bila ya shaka nina mema yangu kwake!' Basi kwa yakini tutawaelezea wale waliokufuru hayo waliyoyatenda, na kwa yakini tutawaonjesha adhabu ngumu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tukimneemesha mwanadamu, hugeuka na kujitenga upande, na inapomgusa shari, huwa na madua marefu marefu.
Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: 'Mnaonaje! Ikiwa haya yanatoka kwa Mwenyezi Mungu, nanyi ikawa ndio mmeyakataa, ni nani aliyepotea zaidi kuliko aliye katika upinzani wa mbali?'
Swahili Translation - Rowad Translation CenterTutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli. Je, haikutoshi kwamba Mola wako Mlezi kuwa Yeye ni Shahidi bora wa kila kitu?
Swahili Translation - Rowad Translation CenterTanabahi, hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Mola wao Mlezi! Tanabahi, hakika Yeye amekizingira kila kitu.