caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Ankaboot, Aya 46

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 85 · 29:46

وَلَا تُجَٰدِلُوٓا۟ أَهْلَ ٱلْكِتَٰبِ إِلَّا بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ مِنْهُمْ وَقُولُوٓا۟ ءَامَنَّا بِٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَأُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَإِلَٰهُنَا وَإِلَٰهُكُمْ وَٰحِدٌ وَنَحْنُ لَهُۥ مُسْلِمُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWala msijadiliane na Watu wa Kitabu isipokuwa kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Na semeni, "Tumeyaamini yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwenu. Na mungu wetu na mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWala msijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia iliyo nzuri kabisa, isipo kuwa wale walio dhulumu miongoni mwao. Na semeni: Tumeyaamini yaliyo teremshwa kwetu na yaliyo teremshwa kwenu. Na Mungu wetu na Mungu wenu ni Mmoja. Na sisi ni wenye kusilimu kwake.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70