وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَنُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّـَٔاتِهِمْ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَحْسَنَ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale walioamini na wakatenda mema, kwa yakini tutawafutia makosa yao, na bila shaka tutawalipa bora ya waliyokuwa wakiyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa walio amini na wakatenda mema, kwa yakini tutawafutia makosa yao, na tutawalipa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.