وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَآ إِلَيْكَ ٱلْكِتَٰبَ فَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَٰهُمُ ٱلْكِتَٰبَ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ وَمِنْ هَٰٓؤُلَآءِ مَن يُؤْمِنُ بِهِۦ وَمَا يَجْحَدُ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَّا ٱلْكَٰفِرُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa namna hivyo tumekuteremshia Kitabu hiki (Qur-ani). Basi wale tuliowapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur-ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakaoiamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipokuwa makafiri.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa namna hivi tumekuteremshia Kitabu (cha Qur'ani). Basi wale tulio wapa Kitabu (cha Biblia) wataiamini (Qur'ani), na miongoni mwa hawa (washirikina) wapo watakao iamini. Na hawazikatai Ishara zetu isipo kuwa makafiri.