وَوَصَّيْنَا ٱلْإِنسَٰنَ بِوَٰلِدَيْهِ حُسْنًا وَإِن جَٰهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِى مَا لَيْسَ لَكَ بِهِۦ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَآ إِلَىَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tumemuusia mwanadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watapambana nawe ili unishirikishe Mimi na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Kwangu Mimi ndiyo marejeo yenu, na nitawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tumemuusia mwanaadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watakushikilia unishirikishe Mimi na usiyo kuwa na ujuzi nayo, basi usiwat'ii. Kwangu Mimi ndio marejeo yenu, na nitakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.