وَلَمَّآ أَن جَآءَتْ رُسُلُنَا لُوطًا سِىٓءَ بِهِمْ وَضَاقَ بِهِمْ ذَرْعًا وَقَالُوا۟ لَا تَخَفْ وَلَا تَحْزَنْ إِنَّا مُنَجُّوكَ وَأَهْلَكَ إِلَّا ٱمْرَأَتَكَ كَانَتْ مِنَ ٱلْغَٰبِرِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wajumbe wetu walipomfikia Luti, alihuzunika kwa sababu yao, na moyo ukaona dhiki kubwa kwa sababu yao. Wakasema, "Usihofu, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, isipokuwa mkeo aliye miongoni mwa watakaokaa nyuma.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa wajumbe wetu walipo mfikia Luut'i, alihuzunika kwa ajili yao, na moyo uliona dhiki kwa ajili yao. Wakasema: Usiogope, wala usihuzunike. Hakika sisi tutakuokoa wewe na ahali zako, ila mkeo aliye miongoni mwa watao kaa nyuma.