وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ ٱلْجَنَّةِ غُرَفًا تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَا نِعْمَ أَجْرُ ٱلْعَٰمِلِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao wameamini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Bustani ya mbinguni yenye kupitiwa chini yake mito, wakidumu humo. Ni mzuri ulioje huo ujira wa watendao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ambao wameamini na wakatenda mema, bila ya shaka tutawaweka katika maghorofa ya Peponi yenye kupitiwa chini yake mito, wakidumu humo. Ni mwema ulioje huo ujira wa watendao.