وَمِنَ ٱلنَّاسِ مَن يَقُولُ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ فَإِذَآ أُوذِىَ فِى ٱللَّهِ جَعَلَ فِتْنَةَ ٱلنَّاسِ كَعَذَابِ ٱللَّهِ وَلَئِن جَآءَ نَصْرٌ مِّن رَّبِّكَ لَيَقُولُنَّ إِنَّا كُنَّا مَعَكُمْ أَوَلَيْسَ ٱللَّهُ بِأَعْلَمَ بِمَا فِى صُدُورِ ٱلْعَٰلَمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika watu yupo yule anayesema, "Tumemuamini Mwenyezi Mungu." Lakini anapopewa maudhi kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, anayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapokuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi, kwa yakini husema, "Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi." Kwani Mwenyezi Mungu hayajui zaidi yaliyomo vifuani mwa walimwengu?
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa katika watu wapo wanao sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu. Lakini wanapo pewa maudhi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wanayafanya mateso ya watu kama ni adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na inapo kuja nusura kutoka kwa Mola wako Mlezi husema: Hakika sisi tulikuwa pamoja nanyi. Kwani Mwenyezi Mungu hayajui yaliomo vifuani mwa walimwengu?