Mwanzo › Sura › Sura Al-Fajr
Sura Al-Fajr الفجر
Aya 30 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 10
بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلْفَجْرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ninaapa kwa alfajiri.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَيَالٍ عَشْرٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa masiku kumi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلشَّفْعِ وَٱلْوَتْرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱلَّيْلِ إِذَا يَسْرِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na kwa usiku unapopita.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
هَلْ فِى ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِى حِجْرٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Je, hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowafanya kina A'di?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِرَمَ ذَاتِ ٱلْعِمَادِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wa Iram, wenye majumba marefu?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّتِى لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِى ٱلْبِلَٰدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُوا۟ ٱلصَّخْرَ بِٱلْوَادِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Thamudi waliochonga majabali huko bondeni?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَفِرْعَوْنَ ذِى ٱلْأَوْتَادِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na Firauni mwenye vigingi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱلَّذِينَ طَغَوْا۟ فِى ٱلْبِلَٰدِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ambao walifanya jeuri katika nchi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَكْثَرُوا۟ فِيهَا ٱلْفَسَادَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wakakithirisha humo ufisadi?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلْمِرْصَادِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَأَمَّا ٱلْإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكْرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَكْرَمَنِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ama mtu anapojaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَهَٰنَنِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ama anapomjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّا بَل لَّا تُكْرِمُونَ ٱلْيَتِيمَ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hamhimizani kulisha masikini.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتَأْكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَتُحِبُّونَ ٱلْمَالَ حُبًّا جَمًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Sivyo hivyo! Itakapovunjwa ardhi vipande vipande.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَجِا۟ىٓءَ يَوْمَئِذٍۭ بِجَهَنَّمَ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكْرَىٰ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini?
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَقُولُ يَٰلَيْتَنِى قَدَّمْتُ لِحَيَاتِى
Swahili Translation - Rowad Translation Center Atasema: Laiti ningelijitangulizia kwa uhai wangu!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
يَٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفْسُ ٱلْمُطْمَئِنَّةُ
Swahili Translation - Rowad Translation Center Ewe nafsi iliyotua!
Tazama tafsiri zote za aya hii →
ٱرْجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً
Swahili Translation - Rowad Translation Center Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umeridhiwa.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
فَٱدْخُلِى فِى عِبَٰدِى
Swahili Translation - Rowad Translation Center Basi ingia miongoni mwa waja wangu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
وَٱدْخُلِى جَنَّتِى
Swahili Translation - Rowad Translation Center Na ingia katika Bustani yangu.
Tazama tafsiri zote za aya hii →
← Sura Al-Ghaashiya
Sura Al-Balad →
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
→
Matini ya Kiarabu na tafsiri kupitia Tanzil na QuranEnc — kama zilivyo, bila kubadilishwa · Tafsiri ni mali ya watafsiri wake na si Qur'ani yenyewe
Hii ni nyenzo ya utafiti, si chanzo cha fatwa.