caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Ghaashiya الغاشية

Aya 26 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 68

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْغَٰشِيَةِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, imekufikia habari ya Msiba wa kufudikiza?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَٰشِعَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku hiyo nyuso zitainama.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterZikifanya kazi, nazo taabani.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً

Swahili Translation - Rowad Translation CenterZiingie katika Moto unaowaka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ ءَانِيَةٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterZikinyweshwa kutoka chemchemi inayochemka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawatakuwa na chakula isipokuwa kichungu chenye miba.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِى مِن جُوعٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakinenepeshi wala hakiondoi njaa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSiku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterZitakuwa radhi kwa juhudi yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika Bustani ya juu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَٰغِيَةً

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHawatasikia humo upuuzi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHumo imo chemchemi inayomiminika.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHumo vimo viti vilivyonyanyuliwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa bilauri zilizopangwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa matakia safu safu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَزَرَابِىُّ مَبْثُوثَةٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mazulia yaliyotandikwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe! Hawamtazami ngamia jinsi alivyoumbwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيْفَ رُفِعَتْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa mbingu jinsi ilivyoinuliwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِلَى ٱلْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa milima jinsi ilivyowekwa imara?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِلَى ٱلْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ardhi jinsi ilivyotandazwa?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَذَكِّرْ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWewe si mwenye kuwatawalia.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini anayerudi nyuma na kukataa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَكْبَرَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBasi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ إِلَيْنَآ إِيَابَهُمْ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70