إِنَّآ أَنزَلْنَا عَلَيْكَ ٱلْكِتَٰبَ لِلنَّاسِ بِٱلْحَقِّ فَمَنِ ٱهْتَدَىٰ فَلِنَفْسِهِۦ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيْهَا وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Kwa hivyo, mwenye kuongoka, ni kwa faida ya nafsi yake. Na mwenye kupotoka, bila ya shaka amepotoka kwa hasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika Sisi tumekuteremshia Kitabu kwa ajili ya watu wote kwa Haki. Basi mwenye kuongoka ni kwa nafsi yake, na mwenye kupotoka bila ya shaka amepotoka kwa khasara yake. Na wewe si mlinzi juu yao.