وَإِن كَادُوا۟ لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ ٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ لِتَفْتَرِىَ عَلَيْنَا غَيْرَهُۥ وَإِذًا لَّٱتَّخَذُوكَ خَلِيلًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika walikaribia kukushawishi uache hayo tuliyokufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo, ndipo wangelikufanya mwandani.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya rafiki.