وَمَن يَهْدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلْمُهْتَدِ وَمَن يُضْلِلْ فَلَن تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِهِۦ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَٰمَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا مَّأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَٰهُمْ سَعِيرًا
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa yule ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoa, basi huyo ndiye aliyeongoka. Na yule ambaye anampotoa, basi hutawapatia walinzi wowote badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kuwa wanakokotwa juu ya nyuso zao, huku ni vipofu, mabubu, na viziwi. Na makazi yao ni Jahannamu. Kila ukifanya kuzimika, tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa anaye mhidi (muongoza) Mwenyezi Mungu basi huyo ndiye aliye hidika. Na anaye wapotoa basi huto wapatia walinzi badala yake. Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.