caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Israa, Aya 60

Makka · mpangilio wa kuteremshwa 50 · 17:60

وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِٱلنَّاسِ وَمَا جَعَلْنَا ٱلرُّءْيَا ٱلَّتِىٓ أَرَيْنَٰكَ إِلَّا فِتْنَةً لِّلنَّاسِ وَٱلشَّجَرَةَ ٱلْمَلْعُونَةَ فِى ٱلْقُرْءَانِ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَٰنًا كَبِيرًا

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa tulipokwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwishawazingira hao watu. Na hatukuifanya ndoto tuliyokuonyesha isipokuwa ni kuwajaribu watu, na mti uliolaaniwa katika Qur-ani. Na tunawahofisha, lakini haiwazidishii isipokuwa uasi mkubwa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tulipo kwambia: Hakika Mola wako Mlezi amekwisha wazunguka hao watu. Na hatukuifanya ndoto tulio kuonyesha ila ni kuwajaribu watu, na mti ulio laaniwa katika Qur'ani. Na tunawahadharisha, lakini haiwazidishii ila uasi mkubwa.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70