إِنَّ ٱلَّذِى فَرَضَ عَلَيْكَ ٱلْقُرْءَانَ لَرَآدُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ قُل رَّبِّىٓ أَعْلَمُ مَن جَآءَ بِٱلْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِى ضَلَٰلٍ مُّبِينٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika yule aliyekulazimisha kuifuata Qur-ani, hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema, "Mola wangu Mlezi ndiye anayemjua zaidi mwenye kuja na uongofu, na ni nani aliyemo katika upotovu ulio dhahiri."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniHakika aliye kulazimisha kuifuata Qur'ani hapana shaka atakurudisha pahala pa marejeo. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuja na uwongofu, na nani aliyomo katika upotofu ulio dhaahiri.