وَدَخَلَ ٱلْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَٰذَا مِن شِيعَتِهِۦ وَهَٰذَا مِنْ عَدُوِّهِۦ فَٱسْتَغَٰثَهُ ٱلَّذِى مِن شِيعَتِهِۦ عَلَى ٱلَّذِى مِنْ عَدُوِّهِۦ فَوَكَزَهُۥ مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ قَالَ هَٰذَا مِنْ عَمَلِ ٱلشَّيْطَٰنِ إِنَّهُۥ عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyeji wake, na akakuta humo wanaume wawili wanapigana - mmoja ni katika watu wake, na mwingine katika maadui zake. Kwa hivyo, yule wa kutoka kwa watu wake akamtaka msaada kumpiga adui yake. Kwa hivyo, Musa akampiga ngumi, na akamuua. Akasema, "Hiki ni katika kitendo cha Shetani. Hakika yeye ni adui, mpotezaji dhahiri."
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyeji wake, na akakuta humo watu wawili wanapigana - mmoja ni katika wenzake, na mwengine katika maadui zake. Yule mwenzake alimtaka msaada kumpiga adui yake. Musa akampiga ngumi, akamuuwa. Akasema: Hiki ni kitendo cha Shet'ani; hakika yeye ni adui, mpotezaji dhaahiri.