فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَكَ فَٱعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَآءَهُمْ وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ ٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata matamanio yao tu. Na ni nani aliyepotea zaidi kumshinda anayefuata matamanio yake bila ya uongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu? Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliye potea zaidi kumshinda anaye fuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.