caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Al-Burooj البروج

Aya 22 · Makka · mpangilio wa kuteremshwa 27

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْبُرُوجِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNinaapa kwa mbingu yenye nyota kubwa kubwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلْيَوْمِ ٱلْمَوْعُودِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa Siku iliyoahidiwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kwa shahidi na kinachoshuhudiwa!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُتِلَ أَصْحَٰبُ ٱلْأُخْدُودِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWameangamizwa watu wa makhandaki.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلْوَقُودِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYenye moto wenye kuni nyingi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWalipokuwa wamekaa hapo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wao ni mashahidi wa yale waliyokuwa wakiwafanyia Waumini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَمَا نَقَمُوا۟ مِنْهُمْ إِلَّآ أَن يُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmbaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kila kitu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُوا۟ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَٰتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا۟ فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ ٱلْحَرِيقِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika waliowafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمْ جَنَّٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْكَبِيرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika walioamini na wakatenda mema watapata Bustani za mbinguni zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterHakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

إِنَّهُۥ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye anayeanzisha na ndiye anayerejesha tena.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلْوَدُودُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ذُو ٱلْعَرْشِ ٱلْمَجِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAtendaye ayatakayo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْجُنُودِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe! Zimekufikia habari za Majeshi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYa Firauni na Thamudi?

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى تَكْذِيبٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterLakini waliokufuru wamo katika kukadhibisha.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطٌۢ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazingira.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

بَلْ هُوَ قُرْءَانٌ مَّجِيدٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterBali hii ni Qur-ani tukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

فِى لَوْحٍ مَّحْفُوظٍۭ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKatika Ubao uliohifadhiwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70