caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ar-Ra'd الرعد

Aya 43 · Madina · mpangilio wa kuteremshwa 96

بِسْمِ ٱللَّهِ ٱلرَّحْمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ الٓمٓر تِلْكَ ءَايَٰتُ ٱلْكِتَٰبِ وَٱلَّذِىٓ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ٱلْحَقُّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤْمِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAlif Laam Miim Raa.[1] Hizi ni Ishara za Kitabu. Na yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ ٱلَّذِى رَفَعَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِى لِأَجَلٍ مُّسَمًّى يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ يُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua juu mbingu bila ya nguzo mnazoziona, kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi, na akatiisha jua na mwezi, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Anaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَهُوَ ٱلَّذِى مَدَّ ٱلْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَٰسِىَ وَأَنْهَٰرًا وَمِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ ٱثْنَيْنِ يُغْشِى ٱلَّيْلَ ٱلنَّهَارَ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNaye ndiye aliyeikunjua ardhi na akaweka humo milima mathubuti na mito. Na katika kila matunda akafanya jozi, cha kiume na cha kike. Huufunika usiku juu ya mchana. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kaumu wanaotafakari.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَفِى ٱلْأَرْضِ قِطَعٌ مُّتَجَٰوِرَٰتٌ وَجَنَّٰتٌ مِّنْ أَعْنَٰبٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَآءٍ وَٰحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِى ٱلْأُكُلِ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَٰتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa katika ardhi vimo vipande vilivyokaribiana, na zipo bustani za mizabibu, na mimea mingine, na mitende yenye kuchipua kwenye shina moja na isiyochipua kwenye shina moja, nayo inanyweshwa katika maji yale yale. Na tunaifanya baadhi yake kuwa bora kuliko mingine katika kula. Hakika katika hayo zimo ishara kwa kaumu wanaotia mambo akilini.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا أَءِنَّا لَفِى خَلْقٍ جَدِيدٍ أُو۟لَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِرَبِّهِمْ وَأُو۟لَٰٓئِكَ ٱلْأَغْلَٰلُ فِىٓ أَعْنَاقِهِمْ وَأُو۟لَٰٓئِكَ أَصْحَٰبُ ٱلنَّارِ هُمْ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Je, tukishakuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio waliomkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watakaokuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِٱلسَّيِّئَةِ قَبْلَ ٱلْحَسَنَةِ وَقَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِمُ ٱلْمَثُلَٰتُ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ لِّلنَّاسِ عَلَىٰ ظُلْمِهِمْ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanakuharakisha ulete mabaya kabla ya mazuri, hali ya kuwa zimekwishapita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦٓ إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرٌ وَلِكُلِّ قَوْمٍ هَادٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru wanasema: Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji tu, na kila kaumu ina wa kuwaongoza.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَحْمِلُ كُلُّ أُنثَىٰ وَمَا تَغِيضُ ٱلْأَرْحَامُ وَمَا تَزْدَادُ وَكُلُّ شَىْءٍ عِندَهُۥ بِمِقْدَارٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu anajua mimba ibebwayo na kila cha kike, na kinachopunguka na kuzidi matumboni mwa uzazi. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

عَٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ ٱلْكَبِيرُ ٱلْمُتَعَالِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana, Mkubwa, Mtukufu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَوَآءٌ مِّنكُم مَّنْ أَسَرَّ ٱلْقَوْلَ وَمَن جَهَرَ بِهِۦ وَمَنْ هُوَ مُسْتَخْفٍۭ بِٱلَّيْلِ وَسَارِبٌۢ بِٱلنَّهَارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNi sawa anayeficha kauli yake miongoni mwenu na anayeidhihirisha, na anayejibanza usiku na anayetembea jahara mchana.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَهُۥ مُعَقِّبَٰتٌ مِّنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِۦ يَحْفَظُونَهُۥ مِنْ أَمْرِ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوْمٍ سُوٓءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُۥ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterKila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyoko kwa kaumu mpaka wabadilishe wao yaliyo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anapowatakia kaumu ubaya, basi hakuna cha kuuzuia wala hawana mlinzi yeyote asiyekuwa Yeye.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

هُوَ ٱلَّذِى يُرِيكُمُ ٱلْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنشِئُ ٱلسَّحَابَ ٱلثِّقَالَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterYeye ndiye anayewaonyesha umeme kwa hofu na matumaini, na huyaanzisha mawingu mazito.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيُسَبِّحُ ٱلرَّعْدُ بِحَمْدِهِۦ وَٱلْمَلَٰٓئِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِۦ وَيُرْسِلُ ٱلصَّوَٰعِقَ فَيُصِيبُ بِهَا مَن يَشَآءُ وَهُمْ يُجَٰدِلُونَ فِى ٱللَّهِ وَهُوَ شَدِيدُ ٱلْمِحَالِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa radi inamtakasa Mwenyezi Mungu kwa kumsifu, na Malaika pia, kwa kumhofu. Naye hutuma mapigo ya radi na kumsibu kwayo amtakaye. Nao wanabishana kuhusiana na Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye adhabu kali!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَهُۥ دَعْوَةُ ٱلْحَقِّ وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسْتَجِيبُونَ لَهُم بِشَىْءٍ إِلَّا كَبَٰسِطِ كَفَّيْهِ إِلَى ٱلْمَآءِ لِيَبْلُغَ فَاهُ وَمَا هُوَ بِبَٰلِغِهِۦ وَمَا دُعَآءُ ٱلْكَٰفِرِينَ إِلَّا فِى ضَلَٰلٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWa kuombwa kweli ni Yeye tu. Na hao wanaowaomba badala yake hawawajibu chochote; bali ni kama mwenye kunyoosha viganja vyake kwenye maji ili yafike kinywani mwake, lakini hayakifikii. Na maombi ya makafiri hayako isipokuwa katika upotovu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلِلَّهِ يَسْجُدُ مَن فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَٰلُهُم بِٱلْغُدُوِّ وَٱلْـَٔاصَالِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi kwa kutii na kwa lazima. Na pia vivuli vyao, asubuhi na jioni.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

قُلْ مَن رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ قُلِ ٱللَّهُ قُلْ أَفَٱتَّخَذْتُم مِّن دُونِهِۦٓ أَوْلِيَآءَ لَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ نَفْعًا وَلَا ضَرًّا قُلْ هَلْ يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ أَمْ هَلْ تَسْتَوِى ٱلظُّلُمَٰتُ وَٱلنُّورُ أَمْ جَعَلُوا۟ لِلَّهِ شُرَكَآءَ خَلَقُوا۟ كَخَلْقِهِۦ فَتَشَٰبَهَ ٱلْخَلْقُ عَلَيْهِمْ قُلِ ٱللَّهُ خَٰلِقُ كُلِّ شَىْءٍ وَهُوَ ٱلْوَٰحِدُ ٱلْقَهَّٰرُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterSema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu na ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, mnawafanya wenginewe badala yake kuwa ni walinzi, nao hawajimilikii manufaa yoyote wala madhara? Sema: Je, kipofu na mwenye kuona huwa sawa? Au je, huwa sawa giza na mwangaza? Au wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika walioumba kama alivyoumba Yeye, na viumbe hivyo vikawachanganyikia? Sema: Mwenyezi Mungu ndiye Muumba wa kila kitu. Na Yeye ni Mmoja, Mwenye kushinda!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌۢ بِقَدَرِهَا فَٱحْتَمَلَ ٱلسَّيْلُ زَبَدًا رَّابِيًا وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيْهِ فِى ٱلنَّارِ ٱبْتِغَآءَ حِلْيَةٍ أَوْ مَتَٰعٍ زَبَدٌ مِّثْلُهُۥ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْحَقَّ وَٱلْبَٰطِلَ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَآءً وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمْكُثُ فِى ٱلْأَرْضِ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْأَمْثَالَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmeteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kiasi chake. Na mafuriko yakabeba mapovu yaliyokusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyoyeyusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano ya haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu. Na ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivyo ndivyo anavyopiga Mwenyezi Mungu mifano.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لِلَّذِينَ ٱسْتَجَابُوا۟ لِرَبِّهِمُ ٱلْحُسْنَىٰ وَٱلَّذِينَ لَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُۥ لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفْتَدَوْا۟ بِهِۦٓ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ سُوٓءُ ٱلْحِسَابِ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata mazuri. Na wale ambao hawakumuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea! Hao wana hesabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni mahali pabaya mno pa kupumzikia!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَن يَعْلَمُ أَنَّمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ٱلْحَقُّ كَمَنْ هُوَ أَعْمَىٰٓ إِنَّمَا يَتَذَكَّرُ أُو۟لُوا۟ ٱلْأَلْبَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, anayejua ya kwamba yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki ni sawa na aliye kipofu? Hakika wenye akili ya hali ya juu tu ndio wanaokumbuka.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ يُوفُونَ بِعَهْدِ ٱللَّهِ وَلَا يَنقُضُونَ ٱلْمِيثَٰقَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale ambao wanatimiza mapatano yao na Mwenyezi Mungu, wala hawavunji agano.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ يَصِلُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ وَيَخَافُونَ سُوٓءَ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale ambao huyaunga yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanamhofu Mola wao Mlezi, na wanaiogopa hesabu mbaya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُوا۟ مِمَّا رَزَقْنَٰهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِٱلْحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ عُقْبَى ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao husubiri kwa kuutaka uso wa Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa katika vile tulivyowapa, kwa siri na kwa uwazi, na wanayaondoa mabaya kwa mazuri. Hao ndio wana malipo ya nyumba nzuri ya Akhera.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

جَنَّٰتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَن صَلَحَ مِنْ ءَابَآئِهِمْ وَأَزْوَٰجِهِمْ وَذُرِّيَّٰتِهِمْ وَٱلْمَلَٰٓئِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِم مِّن كُلِّ بَابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNazo ni Bustani za milele, wataziingia wao na wale waliotengenea miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika watawaingilia katika kila mlango.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

سَلَٰمٌ عَلَيْكُم بِمَا صَبَرْتُمْ فَنِعْمَ عُقْبَى ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation Center(Wakiwaambia) Assalamu Alaikum (Amani iwe juu yenu), kwa sababu ya vile mlivyosubiri! Basi ni mema mno malipo ya Nyumba ya Akhera.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوٓءُ ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale wanaovunja agano la Mwenyezi Mungu baada ya kulifunga, na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya uharibifu katika ardhi, hao wana laana, na wana Nyumba mbaya.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱللَّهُ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ وَفَرِحُوا۟ بِٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِلَّا مَتَٰعٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na waliufurahia uhai wa dunia. Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ قُلْ إِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِىٓ إِلَيْهِ مَنْ أَنَابَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wanasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa anayerudi kwake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ ٱللَّهِ أَلَا بِذِكْرِ ٱللَّهِ تَطْمَئِنُّ ٱلْقُلُوبُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumtaja Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumtaja Mwenyezi Mungu ndiyo nyoyo hutua!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ طُوبَىٰ لَهُمْ وَحُسْنُ مَـَٔابٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale walioamini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَٰكَ فِىٓ أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهَآ أُمَمٌ لِّتَتْلُوَا۟ عَلَيْهِمُ ٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِٱلرَّحْمَٰنِ قُلْ هُوَ رَبِّى لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNdivyo hivyo tulivyokutuma kwa umma ambao zimekwishapita kabla yao umma nyingine, ili uwasomee yale tuliyokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani (Mwingi wa Rehema)! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndiyo marejeo!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَوْ أَنَّ قُرْءَانًا سُيِّرَتْ بِهِ ٱلْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ ٱلْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ ٱلْمَوْتَىٰ بَل لِّلَّهِ ٱلْأَمْرُ جَمِيعًا أَفَلَمْ يَا۟يْـَٔسِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَهَدَى ٱلنَّاسَ جَمِيعًا وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُوا۟ قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِّن دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِىَ وَعْدُ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخْلِفُ ٱلْمِيعَادَ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama ingelikuwako Qur-ani inayoendeshewa milima, na kupasuliwa kwayo ardhi, na kusemeshwa kwayo wafu, (basi ingelikuwa Qur-ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, bila ya shaka angeliwaongoa watu wote? Na wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa yale waliyoyatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدِ ٱسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَمْلَيْتُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako. Na nikawapururia wale waliokufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَفَمَنْ هُوَ قَآئِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفْسٍۭ بِمَا كَسَبَتْ وَجَعَلُوا۟ لِلَّهِ شُرَكَآءَ قُلْ سَمُّوهُمْ أَمْ تُنَبِّـُٔونَهُۥ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِى ٱلْأَرْضِ أَم بِظَٰهِرٍ مِّنَ ٱلْقَوْلِ بَلْ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مَكْرُهُمْ وَصُدُّوا۟ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنْ هَادٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika! Sema: Watajeni. Au ndiyo mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu tu? Bali wale waliokufuru wamepambiwa njama zao na wamezuiliwa njia ya sawasawa. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana yeyote wa kumwongoa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

لَّهُمْ عَذَابٌ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَشَقُّ وَمَا لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ مِن وَاقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterWana adhabu katika uhai wa dunia, na adhabu ya Akhera hakuna shaka ndiyo ngumu zaidi. Na wala hawatakuwa na wa kuwalinda kutokana na Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

مَّثَلُ ٱلْجَنَّةِ ٱلَّتِى وُعِدَ ٱلْمُتَّقُونَ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَٰرُ أُكُلُهَا دَآئِمٌ وَظِلُّهَا تِلْكَ عُقْبَى ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوا۟ وَّعُقْبَى ٱلْكَٰفِرِينَ ٱلنَّارُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMfano wa Bustani waliyoahidiwa wacha Mungu, kwa chini yake inapita mito, chakula chake ni cha daima, na pia kivuli chake. Huu ndio mwisho wa wale waliomcha Mungu. Na mwisho wa makafiri ni Moto.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَٰهُمُ ٱلْكِتَٰبَ يَفْرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمِنَ ٱلْأَحْزَابِ مَن يُنكِرُ بَعْضَهُۥ قُلْ إِنَّمَآ أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشْرِكَ بِهِۦٓ إِلَيْهِ أَدْعُوا۟ وَإِلَيْهِ مَـَٔابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale tuliowapa Kitabu wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake. Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe. Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَٰهُ حُكْمًا عَرَبِيًّا وَلَئِنِ ٱتَّبَعْتَ أَهْوَآءَهُم بَعْدَ مَا جَآءَكَ مِنَ ٱلْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن وَلِىٍّ وَلَا وَاقٍ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ndivyo hivyo tumeiteremsha (Qur-ani hii kuwa ni) hukumu kwa lugha ya Kiarabu. Na ukifuata matamanio yao baada ya elimu hii iliyokujia, hutakuwa na rafiki yeyote wala mlinzi kando na Mwenyezi Mungu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَٰجًا وَذُرِّيَّةً وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَن يَأْتِىَ بِـَٔايَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ ٱللَّهِ لِكُلِّ أَجَلٍ كِتَابٌ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa hakika Sisi tulikwishawatuma Mitume kabla yako, na tukawafanya wawe na wake na dhuria. Na haikuwa kwa Mtume yeyote kuleta ishara isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kila kipindi kina hukumu yake iliyoandikwa.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

يَمْحُوا۟ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ وَيُثْبِتُ وَعِندَهُۥٓ أُمُّ ٱلْكِتَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu hufuta na huthibitisha ayatakayo. Na kiko kwake Kitabu asili.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَإِن مَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ ٱلَّذِى نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِنَّمَا عَلَيْكَ ٱلْبَلَٰغُ وَعَلَيْنَا ٱلْحِسَابُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ikiwa tutakuonyesha baadhi ya yale tuliyowaahidi au tukakufisha kabla yake, juu yako wewe ni kufikisha ujumbe tu na juu yetu ni hesabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ أَنَّا نَأْتِى ٱلْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا وَٱللَّهُ يَحْكُمُ لَا مُعَقِّبَ لِحُكْمِهِۦ وَهُوَ سَرِيعُ ٱلْحِسَابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, hawakuona kwamba tunaijia ardhi tukiipunguza kutokea nchani mwake? Na Mwenyezi Mungu huhukumu, na hakuna wa kurekebisha hukumu yake, naye ni Mwepesi wa kuhesabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَقَدْ مَكَرَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلِلَّهِ ٱلْمَكْرُ جَمِيعًا يَعْلَمُ مَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ وَسَيَعْلَمُ ٱلْكُفَّٰرُ لِمَنْ عُقْبَى ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa walipanga njama wale waliokuwa kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye njama zote. Yeye anajua kile inachochuma kila nafsi. Na makafiri watakuja jua ni ya nani nyumba (njema) ya mwisho (huko Akhera)!

Tazama tafsiri zote za aya hii →

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَسْتَ مُرْسَلًا قُلْ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًۢا بَيْنِى وَبَيْنَكُمْ وَمَنْ عِندَهُۥ عِلْمُ ٱلْكِتَٰبِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale waliokufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye elimu ya Kitabu.

Tazama tafsiri zote za aya hii →

Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70