وَلَوْ أَنَّ قُرْءَانًا سُيِّرَتْ بِهِ ٱلْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ ٱلْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ ٱلْمَوْتَىٰ بَل لِّلَّهِ ٱلْأَمْرُ جَمِيعًا أَفَلَمْ يَا۟يْـَٔسِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَهَدَى ٱلنَّاسَ جَمِيعًا وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُوا۟ قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِّن دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِىَ وَعْدُ ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخْلِفُ ٱلْمِيعَادَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa kama ingelikuwako Qur-ani inayoendeshewa milima, na kupasuliwa kwayo ardhi, na kusemeshwa kwayo wafu, (basi ingelikuwa Qur-ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, bila ya shaka angeliwaongoa watu wote? Na wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa yale waliyoyatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.