لِلَّذِينَ ٱسْتَجَابُوا۟ لِرَبِّهِمُ ٱلْحُسْنَىٰ وَٱلَّذِينَ لَمْ يَسْتَجِيبُوا۟ لَهُۥ لَوْ أَنَّ لَهُم مَّا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا وَمِثْلَهُۥ مَعَهُۥ لَٱفْتَدَوْا۟ بِهِۦٓ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ سُوٓءُ ٱلْحِسَابِ وَمَأْوَىٰهُمْ جَهَنَّمُ وَبِئْسَ ٱلْمِهَادُ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterWale waliomuitikia Mola wao Mlezi watapata mazuri. Na wale ambao hawakumuitikia, hata wangelikuwa na vyote vilivyo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangelivitoa kujikombolea! Hao wana hesabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni mahali pabaya mno pa kupumzikia!
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniWalio muitikia Mola wao Mlezi watapata wema. Na wasio muitikia, hata wangeli kuwa navyo vyote viliomo katika ardhi na mfano wa hivyo, bila ya shaka wangeli vitoa kujikombolea! Hao watapata hisabu mbaya kabisa, na makao yao ni Jahannamu. Na hapo ni pahala pabaya mno!