أَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌۢ بِقَدَرِهَا فَٱحْتَمَلَ ٱلسَّيْلُ زَبَدًا رَّابِيًا وَمِمَّا يُوقِدُونَ عَلَيْهِ فِى ٱلنَّارِ ٱبْتِغَآءَ حِلْيَةٍ أَوْ مَتَٰعٍ زَبَدٌ مِّثْلُهُۥ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْحَقَّ وَٱلْبَٰطِلَ فَأَمَّا ٱلزَّبَدُ فَيَذْهَبُ جُفَآءً وَأَمَّا مَا يَنفَعُ ٱلنَّاسَ فَيَمْكُثُ فِى ٱلْأَرْضِ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْأَمْثَالَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterAmeteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kiasi chake. Na mafuriko yakabeba mapovu yaliyokusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyoyeyusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyopiga mifano ya haki na batili. Basi lile povu linapita kama takataka tu. Na ama kinachowafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivyo ndivyo anavyopiga Mwenyezi Mungu mifano.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniAmeteremsha maji kutoka mbinguni. Na mabonde yakamiminika maji kwa kadiri yake. Na mafuriko yakachukua mapovu yaliyo kusanyika juu yake. Na kutokana na wanavyo yayusha katika moto kwa kutaka mapambo au vyombo hutokea povu vile vile. Namna hivyo Mwenyezi Mungu ndivyo anavyo piga mifano ya Haki na baat'ili. Basi lile povu linapita kama takataka tu basi. Ama kinacho wafaa watu hubakia kwenye ardhi. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga mifano.