أَفَمَنْ هُوَ قَآئِمٌ عَلَىٰ كُلِّ نَفْسٍۭ بِمَا كَسَبَتْ وَجَعَلُوا۟ لِلَّهِ شُرَكَآءَ قُلْ سَمُّوهُمْ أَمْ تُنَبِّـُٔونَهُۥ بِمَا لَا يَعْلَمُ فِى ٱلْأَرْضِ أَم بِظَٰهِرٍ مِّنَ ٱلْقَوْلِ بَلْ زُيِّنَ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مَكْرُهُمْ وَصُدُّوا۟ عَنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَن يُضْلِلِ ٱللَّهُ فَمَا لَهُۥ مِنْ هَادٍ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterJe, anayeisimamia kila nafsi kwa yale iliyoyachuma...? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu washirika! Sema: Watajeni. Au ndiyo mnampa habari ya yale asiyoyajua katika ardhi, au ni maneno matupu tu? Bali wale waliokufuru wamepambiwa njama zao na wamezuiliwa njia ya sawasawa. Na yule ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza, basi hana yeyote wa kumwongoa.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniJe! Anaye isimamia kila nafsi kwa yale iliyo yachuma? Na wamemfanyia Mwenyezi Mungu kuwa na washirika! Sema watajeni. Au ndio mnampa khabari ya yale asiyo yajua katika ardhi; au ni maneno matupu? Bali walio kufuru wamepambiwa vitimbi vyao na wamezuiliwa njia. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha apotee basi hana wa kumwongoa.