caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ar-Ra'd, Aya 22

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 96 · 13:22

وَٱلَّذِينَ صَبَرُوا۟ ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِمْ وَأَقَامُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنفَقُوا۟ مِمَّا رَزَقْنَٰهُمْ سِرًّا وَعَلَانِيَةً وَيَدْرَءُونَ بِٱلْحَسَنَةِ ٱلسَّيِّئَةَ أُو۟لَٰٓئِكَ لَهُمْ عُقْبَى ٱلدَّارِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa ambao husubiri kwa kuutaka uso wa Mola wao Mlezi, na wakasimamisha Swala, na wakatoa katika vile tulivyowapa, kwa siri na kwa uwazi, na wanayaondoa mabaya kwa mazuri. Hao ndio wana malipo ya nyumba nzuri ya Akhera.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa ambao husubiri kwa kutaka radhi ya Mola wao Mlezi, na wakashika Swala, na wakatoa, kwa siri na kwa uwazi, katika tulivyo wapa; na wakayaondoa maovu kwa wema. Hao ndio watakao pata malipo ya Nyumba ya Akhera.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70