caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura Ar-Ra'd, Aya 36

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 96 · 13:36

وَٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَٰهُمُ ٱلْكِتَٰبَ يَفْرَحُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمِنَ ٱلْأَحْزَابِ مَن يُنكِرُ بَعْضَهُۥ قُلْ إِنَّمَآ أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ ٱللَّهَ وَلَآ أُشْرِكَ بِهِۦٓ إِلَيْهِ أَدْعُوا۟ وَإِلَيْهِ مَـَٔابِ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa wale tuliowapa Kitabu wanayafurahia yale yaliyoteremshwa kwako. Na katika makundi mengine wapo wanaoyakataa baadhi yake. Sema: Hakika nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu tu, na wala nisimshirikishe. Kwake Yeye ndiko ninaitia na kwake Yeye ndiko marejeo.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa tulio wapa Kitabu wanafurahia uliyo teremshiwa. Na katika makundi mengine wapo wanao yakataa baadhi ya haya. Sema: Nimeamrishwa nimuabudu Mwenyezi Mungu, na wala nisimshirikishe. Kuendea kwake Yeye ndiyo ninaita, na kwake Yeye ndio marejeo yangu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70