ٱللَّهُ ٱلَّذِى رَفَعَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ثُمَّ ٱسْتَوَىٰ عَلَى ٱلْعَرْشِ وَسَخَّرَ ٱلشَّمْسَ وَٱلْقَمَرَ كُلٌّ يَجْرِى لِأَجَلٍ مُّسَمًّى يُدَبِّرُ ٱلْأَمْرَ يُفَصِّلُ ٱلْـَٔايَٰتِ لَعَلَّكُم بِلِقَآءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterMwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua juu mbingu bila ya nguzo mnazoziona, kisha akainuka akawa juu ya Kiti cha Enzi, na akatiisha jua na mwezi, kila kimoja kinakwenda kwa muda maalumu. Anaendesha mambo, na anazipambanua Ishara kwa kina ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu Mlezi.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniMwenyezi Mungu aliye ziinua mbingu bila ya nguzo mnazo ziona, ametawala kwenye Ufalme wake, na amefanya jua na mwezi yamt'ii, kila kimoja kinakwenda kwa kiwango maalumu. Anayapanga mambo, na anazipambanua Ishara ili mpate kuwa na yakini kukutana na Mola wenu Mlezi.