caseriqUtafutaji wa maana katika Qur'ani

Sura At-Tawba, Aya 118

Madina · mpangilio wa kuteremshwa 113 · 9:118

وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُوا۟ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ ٱلْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوٓا۟ أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ

Swahili Translation - Rowad Translation CenterNa pia wale watatu walioachwa nyuma hata ardhi wakaiona kuwa ni finyu juu yao, pamoja na ukunjufu wake, na nafsi zao zikawabana, na wakayakinika kuwa hakuna kimbilio kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake Yeye. Kisha akawakubalia toba ili nao watubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukubali toba sana, Mwenye kurehemu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniNa pia wale watatu walio achwa nyuma hata dunia wakaiona dhiki juu ya ukunjufu wake, na nafsi zao zikabanika, na wakayakinika kuwa hapana pa kumkimbia Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwake Yeye. Kisha akawaelekea kwa rehema yake ili nao waendelee kutubu. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.
Unatafuta mada? Jaribu utafutaji wa maana — swali lako hutafutwa katika aya zote 6,236.
Lugha — 70