كَيْفَ يَكُونُ لِلْمُشْرِكِينَ عَهْدٌ عِندَ ٱللَّهِ وَعِندَ رَسُولِهِۦٓ إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّمْ عِندَ ٱلْمَسْجِدِ ٱلْحَرَامِ فَمَا ٱسْتَقَٰمُوا۟ لَكُمْ فَٱسْتَقِيمُوا۟ لَهُمْ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَّقِينَ
Swahili Translation - Rowad Translation CenterVipi washirikina watakuwa na agano kwa Mwenyezi Mungu na kwa Mtume wake, isipokuwa wale mliofanya agano nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu watawawia wanyoofu, basi nanyi pia wawieni wanyoofu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wacha Mungu.
Swahili Translation - Ali Mohsin Al-BarwaniItakuwaje iwepo ahadi na washirikina mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya Mtume wake, ila wale mlio ahidiana nao kwenye Msikiti Mtakatifu? Basi maadamu wanakwenda nanyi sawa, nanyi pia nendeni sawa nao. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wachamngu .